Pata taarifa kuu
UGANDA-CORONA-AFYA

Serikali ya Uganda yatathmini uwezekano wa kulegeza masharti ya watu kutembea

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema hivi karibuni atatangaza iwapo atalegeza masharti ya watu kukaa nyumbani kutokana na mamabukizi ya Corona, katika taifa hilo ambalo limeshuhudia maambukizi ya watu 79.

Raisa w Uganda Yoweri Museveni  awatahadharisha Waganda kuhusu ugonjwa wa Covid-19.
Raisa w Uganda Yoweri Museveni awatahadharisha Waganda kuhusu ugonjwa wa Covid-19. ©Gaël Grilhot/RFI
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo rais Yoweri Museveni ametangaza hatua mpya za kudhibiti mienendo ya madereva wa malori yanayoingia nchini humo kutoka mataifa jirani baada ya zaidi ya madereva 20 kupatikana na ugonjwa wa Covid-19.

Hatua hizo ni pamoja na kila lori kuwa na mtu mmoja - dereva pekee yake ambaye hataruhusiwa kulala hotelini wala nyumbani kwa watu.

Katika hotuba yake kwa taifa usiku wa Jumanne rais Museveni amebaini kwamba madereva hao ni tishio katika mapambano ya nchi hiyo dhidi ya Corona akitoa mfano wa janga la Ukimwi la miaka ya 1980 na miaka ya tisini wakati ambapo madereva wa malori katika kanda hiyo waliaambukiza watu virus vya HIV katika kila miji waliyopitia wakiwa safarini.

Muda wa watu kubaki nyumbani unamalizika tarehe 5 Mei 2020.

Wakati hayo yakijiri Shirika la Kimataifa la Kutoa Misaada (IRC) limeonya kuwa watu bilioni moja huenda wakaambukizwa virusi vya Corona kote duniani, huku likisema nchi zisizojiweza zinahitaji usaidizi wa haraka.

Nalo Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeonya kuwa mataifa  tisa ya Afrika Mashariki yapo katika hatari ya kukabiliwa na ukosefu wa chakula cha kutosha kutokana na janga la Corona.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.