Pata taarifa kuu
RWANDA-HAKI

Rwanda: Tom Byabagamba ashtumiwa kutaka kutoroka jela, ndugu zake wakamatwa

Nchini Rwanda, watu watatu wamekamatwa wakishtumiwa kushiriki katika jaribio la kumtorosha Tom Byabagamba, mkuu wa zamani wa kikosi cha ulinzi wa rais Paul Kagame.

Jenerali Frank Rusagara (kulia) na kolonel Tom Byabagamba (kushoto) mbele ya Mahakama ya kijeshi ya Rwanda.
Jenerali Frank Rusagara (kulia) na kolonel Tom Byabagamba (kushoto) mbele ya Mahakama ya kijeshi ya Rwanda. RFI/Bryson Bichwa
Matangazo ya kibiashara

Tom Byabagamba anashikiliwa katika kambi ya jeshi ya Kanombe. Alikamatwa mnamo mwaka wa 2014 na kupatikana na hatia, pamoja na shemeji yake Fred Rusagara, ya kuchochea machafuko na kuikashifu bendera ya taifa.

Tom Byabagamba alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 21 jela na shemeji yake Fred Rusagara mika 20 jela. Hukumu ambazo zilipunguzwa hadi miaka kumi na tano mwezi Desemba mwaka jana katika Mahakama ya Rufaa.

Ofisi ya Uchunguzi ya Rwanda inathibitisha kukamatwa kwa watu hao watatu wanaohusishwa katika kesi ya Byabagamba, kati ya Aprili 15 na 17. Ni Jimmy Mugisha, Emmanuel Mukimbiri na John Museminali, ndugu wa Kanali wa zamani katika kikosi cha ulinzi wa rais Paul Kagame.

John Museminali, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Rwanda, ni mume wa Rosemary Museminali, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na dada wa mke wa Tom Byabagamba.Wote watatu wanashtakiwa kwa kosa la "kujaribu kusaidia kutoroka kwa mfungwa".

Katika taarifa iliyotolewa Aprili 9, jeshi lilihakikisha kwamba Tom Byabagamba anatuhumiwa kuwa alijaribu kutoroka jela, na wakati huo jeshi lilitangaza kwamba linachunguza ili kuwapata watu walioshiriki katika mkasa huo.

Hata hivyo katika mashtaka mapya yaliyopewa jina la "bandia" na ndugu wa Tom Byabagamba, David Himbara, katika taarifa iliyochapishwa kwenye blogi, mwanasiasa huyu aliyejitenga na utawala wa Paul Kagame ambaye anaishi uhamishoni, ameelezea kuhusu "ishara mbaya" na kusema ana wasiwasi juu ya maisha ya kaka yake.

Tangu kukamatwa kwake mnamo mwaka wa 2014, Tom Byabagamba na mshitakiwa mwenzake Fred Rusagara wameendelea kubaini kwamba hawana hatia yoyote, huku timu ya maafisa wa Umoja wa Mataifa ikielezea kifungo chao kama cha kisiasa.

Baada ya kupoteza rufaa Desemba 2019, walitoa malalamiko yao mwezi wa Februari mbele ya Mahakama ya Sheria ya Afrika Mashariki (EYCS).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.