Pata taarifa kuu
RWANDA-DRC,USALAMA

Maswali yaibuka kuhusu jeshi la Rwanda kuendesha vita DRC

Maswali yameibuka kuhusu iwapo jeshi la Rwanda limeanzisha vita nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya askari wake kuonekana kwa miezi kadhaaa nchini DRC.

Askari wa Rwanda huko DRC,  Januari 2009. (Picha kumbukumbu)
Askari wa Rwanda huko DRC, Januari 2009. (Picha kumbukumbu) LIONEL HEALING / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ni zaidi ya mwaka mmoja sasa jeshi la Rwanda linashtumiwa kuendesha operesheni zkatika ardhi ya DRC dhidi ya makundi ya waasi ya Rwanda, kwa makubaliano na serikali ya Kinshasa.

Vyama vya upinzani na mashirika ya kiraia nchini Rwanda, na yale ya DRC, yanalaani athari za kitendo cha serikali ya Rwanda kuingiza majeshi yake na kusababisha migongano ya kila mara kati ya raia wa nchi hizo mbili.

Hata hivyo mashirika na vyama vya upinzani katika nchi hizo mbili wameshtumu jumuiya ya kimataifa kukaa kimya. Wakati huo serikali za Kigali na Kinshasa zimeendelea kukanusha madai hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.