Pata taarifa kuu
SUDANI-KUSINI-SIASA-USALAMA

Serikali ya umoja wa kitaifa yatangazwa Sudani Kusini

Hatimaye rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ametangaza majina ya mawaziri wapya watakaounda serikali ya Umoja wa kitaifa nchini humo. Sudan Kusini inakabiliwa na changa moto nyingi kwa kurejesha amani na usalama katika maeneo mbalimbali nchini humo.

Salva Kiir na Riek Machar.
Salva Kiir na Riek Machar. REUTERS/Jok Solomun
Matangazo ya kibiashara

Kwa jumla, serikali hiyo itaundwa na mawaziri 34 na manaibu waziri 10 na wanawake walioteuliwa katika nafasi muhimu.

Wanawake wanane watashiriki katika serikali hiyo ya Sudani Kusini. Mkewe Makamu rais Riek Machar, Angelina Teny, ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi, ni miongoni mwa wanawake hao walioteuliwa kwenye nyadhifa kubwa.

BΓ©atrice Khamisa pia ameteuliwa kuwa Waziri wa mambo ya Nje wa Sudan Kusini. Ni mara ya kwanza nchini Sudan Kusini wanawake kushikilia nafasi kama hizo.

Mwanamke mwingine ameteuliwa kuwa Waziri wa Mazingira.

Upande wa wanaume, Jean-Luc Jock sasa anashikilia wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Afrika, Paul Ayom Akek ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Miezi kumi na nane ilikuwa muhimu kwa Salva Kirr na Riek Machar kukubaliana juu ya masharti ya mchakato wa amani na kabla ya kuundwa kwa serikali ilichukua wiki tatu zaidi kwa mahasimu hao wawili kukubaliana juu ya nafasi muhimu katika serikali hiyo.

Hata hivyo makubaliano kati ya wawili hao yalizaa matunda na kupelekea kushuka kwa mapigano na kuwezesha maendeleo hatua kwa hatua kuelekea suluhu ya kisiasa katika wiki za hivi karibuni.

Wakati huo huo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa mwaka moja kwa tume yake nchini Sudan Kusini, Minuss, ikisema kwamba hali katika nchi hiyo "bado ni hatari kwa amani na usalama katika ukanda huo" .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.