Sudani Kusini: Kiir na Mashar wakubaliana kuunda serikali ya muungano
Viongozi wa Sudan Kusini, rais Salva Kiir na mpinzani wake Riek Machar, wamekubaliana kuunda serikali ya muungano Jumamosi Februari 22, 2020.
Imechapishwa:
Wawili hao wamekubaliana hili baada ya mazungumza ya saa kadhaa katika ikulu ya Juba Alhamisi wiki hii.
Tangazo hilo ni hatua kubwa katika kupatikana kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenywe nchini humo vilivyodumu kwa miaka mitano na kuwaua karibu watu 400,000 na kuliharibu kabisa taifa hilo changa kabisa duniani.
Marekani imepongeza hatua hii na kusema Washington iko tayari kuunga mkono serikali hiyo ambayo itamrejesha Machar kama makamu wa kwanza wa rais.
Matumaini ya kuundwa kwa serikali hii yalionekana baada ya rais Kiir kukubali shinikizo za kupunguza idadi ya majimbo kutoka 32 hadi 10.