Pata taarifa kuu
UGANDA-RWANDA-USHIRIKIANO

Mzozo kati ya Rwanda na Uganda: Kagame na Museveni kukutana London

Rais wa Uganda Yoweri Museveni na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame, wanatarajiwa kukutana jijini London nchini Uingereza, pembezoni mwa mkutano kati ya bara la Afrika na Uingereza kujadili hatua ambazo zimepigwa kuhusu kuimarisha uhusiano wa mataifa hayo jirani.

Rais wa Angola Joao Lourenço amezungukwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni (kushoto) na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame (kulia) baada ya kutia saini makubaliano ya kudumisha amani Jumatano Agosti 21, 2019.
Rais wa Angola Joao Lourenço amezungukwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni (kushoto) na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame (kulia) baada ya kutia saini makubaliano ya kudumisha amani Jumatano Agosti 21, 2019. JOAO DE FATIMA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Huu utakuwa ni mkutano wa kwanza kati ya vionvgozi hao wawili tangu mwezi Agosti mwaka uliopita baada ya mkutano uliofanyika jijini Luanda nchini Angola, walipotia saini mkataba wa kumaliza tofauti zao. Kwenye kikao hicho cha faragha walikuwepo pia mawaziri wa mashauri ya kigeni wa Angola na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, nchi ambazo ni wapatanishi kwenye mzozo huo baina ya Rwanda na Uganda.

Kwenye kikao cha Angola kilichowakutanisha marais wa Uganda, Rwanda,Jamhuri ya Kimokrasia ya Kongo na Kongo Brazzaville marais hao walikubaliana, pamoja na mambo mengine kuundwe tume ya dharura itakayokutana kila mara ili kufanya tathmini ya utekelezwaji wa mkataba huo.

Makubaliano ya Angola yalizitaka pande zote kuheshimu mpaka wa kila nchi pamoja na kuzuia kukamatwa kwa raia wa nchi moja wanaovuka kwenda au kupitia kwenye nchi hiyo kwenda ktk nchi ya tatu.

Hii ilifuatia hali ya kamatakamata ya raia wa Rwanda huko nchini Uganda kwa shutuma za kufanya ujasusi kwa niaba ya serikali suala ambalo siku zote Rwanda imelikanusha na kuitaja Uganda kama inayoendesha njama za kutaka kuhatarisha usalama wa Rwanda kwa kuwapa hifadhi wanaharakati wa kundi la RNC la Kayumba Nyamwasa aliyewahi kuwa mkuu wa majeshi ya Rwanda. Kwa sasa, Nyamwasa yuko uhamishoni nchini Afrika Kusini. Kwa upande wake, Uganda pia inazikanusha tuhuma za Rwanda. Hata hivyo suala la mpaka wa nchi hizo umeendelea kufungwa, huku Rwanda ikiituhumu Uganda kuendelea kuwakamatwa raia wake kiholela, na baadhi yao kupakiwa na kurejeshwa Rwanda kwa nguvu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.