Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-KIIR-AMANI-UBAKAJI

Wasichana na akina mama walibakwa Sudan Kusini kwa siku 10 zilizopita

Shirika la Madaktari wasiokuwa na mipaka, MSF, linasema kwa muda wa siku 10 zilizopita, wanawake na wasichana 125, wamebwakwa nchini Sudan Kusini.

Wanawake nchini Sudan Kusini
Wanawake nchini Sudan Kusini Reuters
Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi wa MSF, umebaini kuwa ubakaji huo ulifanyika wakati wanawake na wasichana hao walipokwenda kupokea chakula cha msaada katika jimbo la Bentiu.

Ruth Okello, mmoja wa Madaktari wa MSF, amesema wiki hii, wanawake na wasichana hao wamekuwa wakitembelea katika kituo chao cha afya wakiwa na wajeraha baada ya kufanyiwa vitendo hivyo vibaya.

Bi. Okello ameongeza kuwa, miongoni mwa waliobakwa ni wasichana walio na chini ya umri wa miaka 10 na wanawake wenye umri wa miaka 65, wakiwemo wajawazito.

Jimbo la Bentiu, limeendelea kuwa miongoni mwa maeneo hatari nchini Sudan Kusini ambayo wanawake wamekuwa wakishambuliwa na kubwa wakati wa vita kati ya makundi ya waasi na wanajeshi wa serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.