Pata taarifa kuu
UGANDA-USALAMA

Moto wavamia mabweni, kumi na moja wafariki Uganda

Wanafunzi kumi na mmoja wamepoteza maisha na wengine 20 wamejeruhiwa vibaya katika mkasa wa moto uliovamia mabweni yao katika shule moja kusini mwa Uganda. Tukio hilo lilitokea siku ya Jumapili usiku, kwa mujibu wa polisi ya Uganda.

Msemaji wa polisi nchini humo Patrick Onyango ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba mamlaka nchini humo zinachunguza ajali hiyo endapo wanafunzi wa zamani wanahusika na uchomaji huo wa shule.
Msemaji wa polisi nchini humo Patrick Onyango ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba mamlaka nchini humo zinachunguza ajali hiyo endapo wanafunzi wa zamani wanahusika na uchomaji huo wa shule. REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

"Wanafunzi kumi na mmoja wamepoteza maisha katika baada ya moto kuzuka katika mabweni matatu ya wavulana katika Shule ya High St. Bernard huko Rakai usiku jana," mkuu wa polisi wa eneo hilo, Ben Nuwamanya aliliambia shirika la Habari la AFP.

"Takribani wanafunzi 20 wamelazwa hospitalini kwa majeruhi makubwa na wana hali mbaya, lakini madaktari wanasema baadhi yao watapona," Ben Nuwamanya ameongeza.

Mkuu wa shule, Henry Nsubuga, amewashtumu baadhi ya wanafunzi waliofukuzwa hivi karibunikuhusika na "kitendo hicho kikatili".

"Wahalifu walifunga kwanza milango ya mabweni kabla ya kutekeleza kitendo hicho kiovu, hata wakati watu waliokuja kutoa msaada, ilikuwa vigumu kuokoa wanafunzi kutoka kwenye mabweni. Baadhi yao waliweza kuokolewa, lakini walifariki kwa kukosa hewa, "Bw Nsubuga amesema.

"Miili mingine iliharibika vibaya kwa moto na mpaka sasa ni vigumu kuitambua. Tayari polisi imeomba kufanyike vipimo vya damu (DNA) ili kuwatambua," Henry Nsubuga ameongeza.

Kwa mujibu wa Bw Nuwamanya, chanzo cha moto huo kinaendelea kuchunguzwa. Polisi imewamata watu watatu, ikiwa ni pamoja na mlinzi wa shule, Ben Nuwamanya amesema.

Viongozi wakuu serikalini, wakiwemo waziri wa elimu, waziri wa ulinzi walisafiri hadi katika shule hiyo ili kujionea uharibifu uliofanywa na moto huo.

Eneo la Rakai linapatikana kwenye umbali wa kilomita 280 kusini magharibi mwa jiji la Kampala, karibu na mpaka na Tanzania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.