Pata taarifa kuu
UGANDA-USALAMA-HAKI

Mkuu wa zamani wa polisi nchini Uganda afikishwa mahakamani

Mkuu wa zamani wa polisi nchini Uganda Jenerali Kale Kayihura amefikishwa katika mahakama ya jeshi ya Makindye baada ya kufunguliwa mashitaka ya kutowajibika katika kazi yake.

Kale Kayihura, aliyekuwa mkuu wa polisi ya Uganda, afikishwa mbele ya Mahakama ya Kijeshi Kampala, Uganda tarehe 24 Agosti 2018.
Kale Kayihura, aliyekuwa mkuu wa polisi ya Uganda, afikishwa mbele ya Mahakama ya Kijeshi Kampala, Uganda tarehe 24 Agosti 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Jenerali Kayihura anakabiliwa na mashitaka mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushindwa kulinda zana za kivita na kusaidia kuhamishwa kiharamu kwa raia wa Rwanda walio uhamishoni.

Kulingana na hati ya mashitaka, kati ya mwaka 2010 na 2018 Kale Kayihura alitoa idhini silaha zitolewe kwa watu wasiostahili

Jenerali Kale Kayihura amefutilia mbali mashitaka dhidi yake akisema kuwa ni madai yasio kuwa na msingi.

Jenerali Kayihura amekuwa akizuiliwa katika kambi ya kijeshi ya Makindye katika kitongoji cha mji mkuu Kampala, baada ya kukamatwa nyumbani kwake Katebe wkatika wilaya ya Lyantonde mnamo mwezi Juni.

Mawakili wake wameomba aachiliwe kwa dhamana, lakini mahakama imewataka wawasilishe ombi hilo kwa maandishi.

Jenerali Kayihura alihudumu kama mkuu wa Polisi kwa takriban miaka 12 kabla ya a kuachishwa kazi na rais Yoweri Kaguta Museveni.

Kesi yake itarudi kusikilizwa tarehe 4 Septemba mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.