Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Odinga asema yuko tayari kuzungumza na rais Kenyatta kuhusu maandalizi ya Uchaguzi

Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amesema yuko tayari kufanya mazungumzo na rais Uhuru Kenyatta kuhusu kufanyika kwa Uchaguzi utakaokuwa huru na haki wala sio namna ya kuunda serikali ya muungano kama inavyodaiwa na rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto.

Raila Odinga akizungumza hivi karibuni katika jumba la siasa la  Chatham jijini London nchini Uingereza Oktoba 13 2017
Raila Odinga akizungumza hivi karibuni katika jumba la siasa la Chatham jijini London nchini Uingereza Oktoba 13 2017 REUTERS/Peter Nicholls
Matangazo ya kibiashara

“Niko tayari kuzungumza na rais Kenyatta kuhusu namna ya kuwa na Uchaguzi utakaokuwa huru na haki sio kuunda serikali ya muungano,” alisema Odinga.

Aidha, amesisitiza kuwa hatawania wadhifa wa urais katika Uchaguzi uliopangwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu bila ya mabadiliko ndani ya Tume ya Uchaguzi.

Rais Kenya na Naibu wake, wamekuwa wakimshutumu Odinga kwa kujiondoa kwenye Uchaguzi huo kwa sababu anataka kuundwa kwa serikali ya muungano.

Mbali na hilo, Mahakama ya Juu nchini Kenya imeamua kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati, hana mamlaka ya kubadilisha matokeo ya Uchaguzi wa urais.

Tume ya Uchaguzi ilikwenda katika Mahakama hiyo kutaka kufahamu jukumu la Mwenyekiti wa Tume hiyo, baada ya matokeo ya urais ya mwezi Agosti kufutwa.

Nayo Mahakama Kuu imeondoa kwa muda marufuku iliyokuwa na serikali kuzuia maandamano ya wafuasi wa upinzani katikati ya miji ya Nairobi, Mombasa na Kisumu.

Upinzani ulienda Mahakamani kutaka kuondolewa kwa marufuku hayo, kwa kile walichosema kuwa ni kinyume na haki za waandamanaji na Katiba ya Kenya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.