Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI

Uhuru Kenyatta: Uchaguzi utafanyika licha ya kujiondoa kwa Odinga

Uamuzi wa kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga wa kujiondoa katika uchaguzi wa Oktoba 26 umewaacha vinywa wazi wananchi wengi wa Kenya hasa wafuasi wa upinzani na baadhi ya wafuasi wa chama tawala cha Jubilee.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anasema Odinga anajidanganya uchaguzi utafanyika tu tarehe 26 Oktoba kama ilivyopangwa.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anasema Odinga anajidanganya uchaguzi utafanyika tu tarehe 26 Oktoba kama ilivyopangwa. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Licha ya hatua hiyo ya mpinzani wake, Rais uhuru Kenyatta amesema uchaguzi utafanyika tarehe 26 kama ilivyopangwa.

hali hii inazua hali ya sintofahamu katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Kwa sasa watu wengi wanajiuliza iwapo uchaguzi wa urais utafanyika au la,au kutakua na mchakato mpya wa uchaguzi, baada ya hatua hii ya kiongozi wa upinzani nchini Kenya.

Hata hivyo kambi ya chama tawala inabaini kwamba uchaguzi utafanika tarehe 26 kama ilivyopangwa au Rais Uhuru Kenyatta atatangazwa moja kwa moja rais wa Kenya.

Wataalamu wa masuala ya sheria ambao wamehojiwa na RFI, wanangazia uamuzi wa Mahakma Kuu wa mwaka 2013, ambao unasema iwapo mmoja kati ya wagombea wawili atajiondoa kabla ya uchaguzi mpya, hali hiyo itasababisha kuandaliwa kwa uchaguzi mpya.

Hali hii inapelekea kuepo na mchakato mpya na zoezi la kuteua wagombea wapya ndani ya muda wa siku 90. hali hiyo itapelekea uchaguzi mpya kufanyika mwezi Januari mwaka, kwa mujibu wa wataalamu hao wa masuala ya sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.