Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI-SIASA

Raila Odinga ajiondoa kwenye uchaguzi wa urais wa Oktoba 26 nchini Kenya

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ametangaza Jumanne hii (Oktoba 10) kwamba anajiondoa kwenye uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Oktoba 26.

Le leader de l'opposition ici à Nairobi le 7 septembre 2017. Raila Odinga a mis en cause l'entreprise française Safran, dont l'ex-filiale Morpho avait fourni les kits de reconnaissance biométrique des électeurs.
Le leader de l'opposition ici à Nairobi le 7 septembre 2017. Raila Odinga a mis en cause l'entreprise française Safran, dont l'ex-filiale Morpho avait fourni les kits de reconnaissance biométrique des électeurs. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Raila Odinga anasema anataka kufanyika uchaguzi mpya jinsi ilivyoamuliwa na Mahakama Kuu.

Kauli hii inakuja siku chache baada ya uchaguzi wa urais kusogezwa mbele hadi Oktoba 26 mwaka huu.

Uchaguzi huo wa tarehe 26 utakuwa ni marudio ya uchaguzi mkuu, baada ya mahakama ya juu nchini Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu.

Uchaguzi huu ulipangwa kufanyika Oktoba 26 kufuatia uamuzi wa Mahakam kuu kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais wa Agosti 8, ambapo rais anaye maliza muda wake alitangazwa mshindi dhidi ya mpinzani wae mkuu Raila Odinga.

Bw. Odinga anasema amefanya hivyo kwa maslahi mazima ya taifa la Kenya na wananchi wake.

"Kwa kuzingatia maslahi ya wananchi wa Kenya, wale wa ukanda huu na dunia kwa ujumla, tunaamini kwamba maslahi ya wote yatatumika vizuri zaidi kwa mimi kutoshiriki uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Oktoba 26, 2017," amesema Raila Odinga katika mkutano na waandishi wa habari mjini Nairobi.

Kwa sasa Uhuru Kenyata ni mgombea pekee ambaye anaonekana kuwa ataliongoza taifa la Kenya kwa muhula wa pili mfululizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.