Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Wanasiasa nchini Kenya wandelea kuvutana kuhusu Uchaguzi mpya wa urais

Wanasiasa nchini Kenya mwishoni mwa juma hili waendelea kuvutana kuhusu Uchaguzi mpya wa urais uliopangwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu.

Raisi Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto, katika Ikulu ya Nairobi.
Raisi Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto, katika Ikulu ya Nairobi. Service de presse de la présidence kényane
Matangazo ya kibiashara

Muungano wa upinzani nchini Kenya, NASA, wameitisha maandamano mapya wiki ijayo kushinikiza mabadiliko ndani ya Tume ya Uchaguzi na kushinikiza wabunge wa chama cha Jubilee kuachana na mchakato wa kubadilisha sheria za Uchaguzi.

Wakati uo, viongozi wa upinzani wameshutumu hatua ya serikali kuwapokonya walinzi wao, kama anavyoeleza Kalonzo Musyoka mmoja wa viongozi wa upinzani.

Serikali imejitetea kwa kusema kuwa imechukua hatua hiyo kwa sababu ya uhaba wa maafisa wa usalama.

Kuhusu maandamano ya upinzani ambayo yatafanyika siku ya Jumatatu, Jumatano na Ijumaa wiki ijayo, Naibu rais Wiliam Ruto amesema, mwafaka hautapatikana kwa njia hiyo.

NASA inasema haitakubali Uchaguzi kufanyika iwapo masharti yao hayatafanyika.

Mataifa ya nje yamewaonya wanasiasa nchini humo kuacha kuchochea raia wa nchi hiyo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.