Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI

Upinzani kumiminika mitaani nchini Kenya

Wafuasi wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, wanatarajiwa kuandamana nchini humo kushinikiza mabadiliko ndani ya Tume ya Uchaguzi kuelekea Uchaguzi mpya wa urais uliopangwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu.

Maandamano ya upinzani jijini Nairobi nchini Kenya
Maandamano ya upinzani jijini Nairobi nchini Kenya Photographer James Shimanyala's - copyright RFI"
Matangazo ya kibiashara

Aidha, wanataka chama cha Jubilee kuacha mchakato wa kubadilisha sheria za Uchaguzi.

Wiki iliyopita, kiongozi wa NASA Raila Odinga alitangaza kuwa maandamano haya, yatakuwa yanafanyika kila Jumatatu na Ijumaa.

Kuelekea katika maandamano haya, Odinga ameshtumu Polisi kwa kuendelea kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya wafuasi wake.

Siku ya Alhamisi mkutano wa chama cha Jubilee ulikumbwa na kizaaza baada ya watu walioshiriki mkutano huo kushambuliwa na nyuki.

Tukio hilo lilitokea katika kaunti ya Taita-Taveta yapata kilomita 360 kutoka mji mkuu wa Nairobi kwa mujibu wa gazeti la The Standard.

Wafuasi wa chama hicho walilazimika kukimbilia usalama wao wakati nyuki hao walipowavamia , lakini wakapotea baada ya maombi kufanywa na mwanasiasa mmoja.

Wanasiasa walilaumu shetani kwa uvamizi huo wa mkutano huo uliofanyika katika mji wa Wundanyi ,ulioitishwa kumuunga mkono rais Uhuru Kenyatta kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.