Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI

Upinzani waitisha maandamano makubwa wiki ijayo nchini Kenya

Muungano wa upinzani nchini Kenya umewataka wafuasi wake kuitikia maandamano makubwa yaliyopangwa kufanyika sikuya Jumatatu wiki ijayo kupinga mapendekezo ya kuifanyia mabadiliko sheria ya uchaguzi.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga hapa ni mjini Nairobi Septemba 7, 2017.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga hapa ni mjini Nairobi Septemba 7, 2017. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Wabunge wa upinzani walitoka nje wakati ambapo wale wa serikali walitumia wingi wao kuharakisha mabadiko ambayo yatasababisha mswada huo kuwa sheria kabla ya marudio ya uchaguzi.

Miongoni mwa yaliyo kwenye mswada huo ni kuruhusu mgombea kutangazwa rais bila ya kufanyika uchaguzi ikiwa mgombea mwingine atasusia uchaguzi.

Mswada huo pia unasema kuwa mahakama ya juu haiwezi kufuta matokeo ikiwa mfumo wa eletroniki utafeli.

Mhakama ya Juu ilichukua uamuzi wa kufuta maotkeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika Agosti kufuatia kufeli kwa mfumo wa kupiga kura kwa njia ya eletroniki .

Katika uchaguzi huu wa marudio wagombea ni wawili, pekee, Rais anayemaliza muda wake Uhuru Kenyatta na kiongozi mkuu wa upinzani Raila Odinga.

Hata hivyo Raila Odinga ametisha maandamano makubwa ambayo yanatazamiwa kufanyika nchini kote siku ya Jumatatu na Ijumaa kuanzia wiki ijayo.

Hata hivyo polisi imeonya kwa watu kuandamana kwa lengo la kuhatarisha usalama wa taifa.

Marudio ya uchaguzi yamepangwa kufanyika tarehe 26 mwezi Oktoba mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.