Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI

Upinzani kuandamana kwenye makao makuu ya IEBC nchini Kenya

Hali ya sintofahamu na mvutano vinaendelea nchini Kenya, baada ya mahakama Kuu nchini humo kutangaza rasmi kufutwa kwa uchaguzi wa urais uliofanyika Agosti 8 mwaka huu. Upinzani nchini Kenya umeitisha maandamano leo Jumanne.

Viongozi wa upinzani wa Kenya Musalia Mudavadi, Kalonzo Musyoka, Raila Odinga, Moses Wetangula na Nick Salat wakiungana Januari 11 huko Nairobi.
Viongozi wa upinzani wa Kenya Musalia Mudavadi, Kalonzo Musyoka, Raila Odinga, Moses Wetangula na Nick Salat wakiungana Januari 11 huko Nairobi. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Chama cha NASA cha Raila Odinga kimesema maandamano hayo yatafanyika nje ya makao makuu ya tume ya uchaguzi IEBC mjini Nairobi.

NASA imekanusha taarifa iliyoelezwa hapo awali kuwa katika maandamano hayo upinzani utovamia makao ya tume ya ya uchaguzi IEBC kuwatimua kwa nguvu maafisa wa tume hiyo. Hata hivyo NASA imebaini kwamba maandamano hayo yatakuwa ya amani.

“Maandamano haya yana lengo la kushinikiza kujiuzulu kwa baadhi ya maafisa wa juu wa tume ya uchaguzi (IEBC) walioshiriki kuandaa uchaguzi mkuu wa Agosti 8 mwaka huu, uchaguzi ambao ulifutwa na Mahakama Kuu nchini, ” NASA imesema kataika taarifa yake.

Muungano wa NASA unataka jumla ya maafisa 12 wa tume hiyo washtakiwe kwa kutowajibika katika uchaguzi uliofutwa wa Agosti 8. Unataka pia mfumo wa teknolojia uliotumiwa wakati wa uchaguzi huo ubadilishwe.

Rais Uhuru Kenyatta ameonya waandamanaji kuwa watakabiliwa na hatua kali za sheria iwapo maandamano yao yatasababisha shughuli za kiuchumi za raia zinakwama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.