Pata taarifa kuu
KENYA-IEBC-UCHAGUZI

Uchaguzi Kenya: Mwendesha Mashitaka Mkuu aagiza uchunguzi katika tume ya uchaguzi

Kiongozi wa mashitaka nchini Kenya Keriako Tobiko, ameagiza kuchunguzwa kwa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya baada ya kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi wa urais mwezi uliopita.

Maofisa wa tume huru ya uchaguzi nchini Kenya, IEBC, wakiwa katika shughuli ya kuandikisha wapiga kura wapya, 16 Januari 2017.
Maofisa wa tume huru ya uchaguzi nchini Kenya, IEBC, wakiwa katika shughuli ya kuandikisha wapiga kura wapya, 16 Januari 2017. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Tobiko ameagiza Polisi na maafisa wa tume ya kupambana na ufisadi kuchunguza iwapo wafanyakazi wa Tume hiyo walihusika na udanganyifu uliosababisha matokeo hayo kufutwa.

Hatua hii inakuja wakati huu kiongozi wa upinzani Raila Odinga akisema hataruhusu kushiriki uchaguzi mpya uliopangwa kufanyika tarehe 26 mwezi Oktoba iwapo Tume ya Uchaguzi haitafanyiwa marekebisho.

Hayo yanajiri wakati Tume ya uchaguzi IEBC hivi karibuni ilitangaza tarehe 26 mwezi Otoba 2017 kama tarehe mpya ya uchaguzi wa marudio.

Tarehe hiyo ilitangazwa ikiwa ni siku tano tu kabla ya kukamilika kwa siku 60 zilizowekwa kikatiba kufanyika kwa uchaguzi mpya.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo IEBC Wafula Chebukati alitangaza kuwa hatua hiyo imechukuliwa ili kuhakikisha kuwatume anayoongoza imejiandaa vilivyo.

Rais anayemaliza muda wake Huru Kenyatta alikua aliibuka mshindi wa uchaguzi wa urais ambao matokeo yake yalifutwa na mMahakama Kuu nchini Kenya.

Serikali ya Kenya ilitoa dola milioni 97 kwa ajili ya uchaguzi huu mpya, ambao iutajadiliwa bungeni siku ya Jumanne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.