Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI

NASA na JUBILEE hawafurahii mabadiliko katika IEBC

Tume ya Uchaguzi nchini Kenya, imewekwa njia panda baada ya Muungano wa upinzani NASA na chama cha Jubilee kusema hawaridhishwi na mabadiliko yaliyofanywa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Wafula Chebukati kuelekea Uchaguzi mpya mwezi ujao

Maofisa wa tume huru ya uchaguzi nchini Kenya, IEBC, wakiwa katika shughuli ya kuandikisha wapiga kura wapya, 16 Januari 2017.
Maofisa wa tume huru ya uchaguzi nchini Kenya, IEBC, wakiwa katika shughuli ya kuandikisha wapiga kura wapya, 16 Januari 2017. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Chama cha Jubilee cha rais Uhuru Kenyatta kinasema watendaji wapya tisa walioteliwa kusimamia Uchaguzi huo mpya wa urais, wanaegemea mrengo wa kisiasa.

Hata hivyo, IEBC imekanusha madai hayo na kusema haitapangiwa cha kufanya kwa sababu ni Tume huru.

Hivi karibuni Mahakama ya Juu nchini Kenya ilitoa uamuzi wa kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais uliyofanyika mwanzoni mwa mwezi Agosti. Uchaguzi ambao uhuru Kenyaata alikua aliibuka mshindi.

Uchaguzi mpya wa Urais nchini humo umepangwa kufanyika Oktoba 17, 2017. Wagombea watakaomenyana katika uchaguzi huo ni Uhuru Kenyatta, rais anaye maliza muda wake, na mpinzani mkuu Raila Odinga, kwa mujibu wa tume huru ya Uchaguzi (IEBC).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.