Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI-HAKI

Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi yasubiriwa Kenya

Majaji wa mahakama ya juu nchini Kenya wanasaidiwa na jopo la watu 40 kupitia nyaraka zaidi ya elfu 70 zilizowasilishwa mahakamani kama ushahidi ili kuwasaidia kuamua kuhusu kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa urais wa Agosti 8.

Upinzani nchini Kenya inaishtumu Tume ya Uchaguzi (EBC) kuhusika katika wizi wa kura.
Upinzani nchini Kenya inaishtumu Tume ya Uchaguzi (EBC) kuhusika katika wizi wa kura. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Majaji hao saba wanasalia na saa chache tu kabla ya hapo kesho kutarajiwa kutoa uamuzi kuhusu kesi iliyowasilishwa na kinara wa upinzani Raila Odinga anayepinga ushindi wa rais Uhuru Kenyatta.

Hukumu ya kesi hii inasubiriwa kwa hamu sio tu na wananchi wa Kenya lakini pia inatazamwa na mataifa mbalimbali duniani, wengi wakisubiri hatma ya kesi hiyo.

Agosti 11 Tume ya Uchaguzi IEBC ilimtangaza Uhuru Kenyatta mshindi kwa kupata asilimia 54.27 huku Raila Odinga akiwa wa pili kwa asilimia 44.74.

Odinga alikataa kuyatambua matokeo hayo, hal iliyozua maandamano ya wafuasi wa upinzani mjini Kisumu, mtaani Mathare na Kibera jijini Nairobi na kusababisha vifo vya watu 21, akiwemo mtoto mchanga na msichana wa miaka tisa.

Muungano wa upinzani NASA, unataka Mahakama kutupilia mbali matokeo yaliyompa ushindi rais Uhuru Kenyatta na kuitisha Uchaguzi mpya ndani ya siku sitini.

Kuthibitisha hili, Mawakili wa upinzani waliiambia Mahakama kuwa Tume ya Uchaguzi ilighushi matokeo yaliyompa Kenyatta ushindi katika fomu za 34 A na 34 B.

Majaji wa Mahakama ya Juu waliagiza kuwa upinzani upewe nafasi ya kuangalia mitambo ya IEBC iliyokuwa na matokeo halisi, lakini James Orengo wakili wa upinzani akasema kuwa hawakupewa nafasi ya kuangalia mitambo hiyo.

Hata hivyo, Tume ya Uchaguzi ilikanusha madai hayo ya upinzani na kujitetea kuwa matokeo waliyotangaza ndiyo yaliyokuwa sahihi kutoka vituo vya kupigia kura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.