Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI

Maamuzi kuhusu kesi ya urais nchini Kenya kutolewa Ijumaa

Mahakama Kuu nchini Kenya linatazamia kutoa uamuzi wake kuhusu kesi iliyowasilishwa na upinzani wa kupinga ushindi wa Uhuru Kenyatta katika uchaguzi uliofanyika Agosti 8.

Polisi Kisumu, tarehe 12 Agosti, wakati wa maandamano ya wafuasi wa Raila Odinga, mgombea wa rais nchini Kenya alieshindwa na kudai kuwa uchaguzi uligubikwa na wizi wa kura.
Polisi Kisumu, tarehe 12 Agosti, wakati wa maandamano ya wafuasi wa Raila Odinga, mgombea wa rais nchini Kenya alieshindwa na kudai kuwa uchaguzi uligubikwa na wizi wa kura. REUTERS/James Keyi
Matangazo ya kibiashara

Muungano wa upinzani nchini Kenya unadai kuwa mitambo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi IEBC ilidukuliwa na matokeo kuvurugwa. Upinzani pia unaituhumu Tume ya taifa ya Uchaguzi kwa kutumia namba za kupigia kura ambazo zilikuwa hazijathibitishwa rasmi.

NASA inaitaka mahakama kuu kubatilisha matokeo ya uchaguzi huo wa urais.

Muungano hu unadai kuwa matokeo ya uchaguzi ya mwezi Agusti yalikuwa na udanganyifu.

Mahakama inayosikiliza kesi hiyo imeruhusu tayari mawakili wa upinzani kuweza kupata Data na vifaa vilivyotumika katika uchaguzi.

Tume ya taifa ya Uchaguzi nchini humo ilimtangaza Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa uchaguzi kwa ushindi wa zaidi ya nusu ya kura zote zilizopigwa na kumshinda mpinzani wake mkubwa, mkongwe wa siasa za upinzani Raila Odinga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.