Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI

Uchaguzi wa urais nchini Kenya kufanyika Oktoba 17

Tume ya Uchaguzi nchini Kenya imetangaza kuwa imepanga kuandaa uchaguzi mpya wa urais tarehe 17 mwezi ujao.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya Wafula Chebukati
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya Wafula Chebukati IEBCKenya
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya Mahakama ya Juu wiki iliyopita, kufuta ushindi wa rais Uhuru Kenyatta baada ya kubaini kuwa kulikuwa na udanganyifu na kuagiza Uchaguzi mpya kufanyika ndani ya siku 60.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi amesema rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa Muungano wa upinzani Raila Odinga ndio wagombea pekee watakaomenyana katika uchaguzi huu mpya.

Mwenyekiti huyo hata hivyo ametoa wito kwa Mahakama ya Juu kutoa hukumu ya kina kuhuhusu kesi iliyowasilishwa na Bw Odinga kupinga ushindi wa kenyatta ili kuiwezesha "tume kutambua maeneo ambayo yanahitaji kuboreshwa katika usimamizi wa uchaguzi mpya".

Wakati huo huo muungano wa upinzani unataka tume hiyo kufanyiwa marekebisho kabla ya uchaguzi huo, na hasa kumlenga Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Ezra Chiloba ambaye wanataka ajiuzulu.

Upande wa chama cha Jubilee unapinga hilo.

Majaji wa mahakama ya juu waliahidi kutoa hukumu kamili kabla ya tarehe 22 mwezi huu.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na IEBC kuhusu uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti, Rais Kenyatta alipata kura 8,203,290 huku naye Raila Odinga akipata kura 6,762,224.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.