Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI-EAC

Uingereza yampongeza Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa tena

Uingereza imempongeza Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kwa mara nyingine kuliongoza taifa la kenya wakati huu muungano Upinzani Nasa wakijiapiza kutokubali matokeo hayo ya uchaguzi.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiwa na naibu wake William Ruto ambao wametangazwa washindi wa uchaguzi wa 2017
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiwa na naibu wake William Ruto ambao wametangazwa washindi wa uchaguzi wa 2017 REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Boris Johnson imepongeza uchaguzi wa kihistoria uliofanyika siku ya jumanne ambao mamilioni ya wakenya walijitokeza kuchagua viongozi.

Hata hivyo Usalama umeimarishwa nchini kenya baada ya watu wasiopungua kumi kupoteza maisha katika maeneo mbalimbali ambayo ni ngome ya upinzani.

Maafisa wa usalama wametawanywa katika maeneo ya nchi hususan katika ngome za upinzani magharibi mwa nchi na mitaa kadhaa jijini Nairobi.

Aidha Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini humo, limelaani hatua ya Polisi kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji na kuitaka kujiepusha kukabiliana na waandamanaji.

Baraza hilo limetoa wito kwa muungano wa NASA kwenda Mahakamani, kupinga ushindi wa rais Kenyatta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.