Pata taarifa kuu
RWANDA-UCHAGUZI

Kagame ashinda asilimia 98 ya kura za uraisi Rwanda

Raisi wa Rwanda Paul Kagame ameshinda uchaguzi uliofanyika ijumaa kwa asilimia 98 ya kura kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotolewa na tume ya uchaguzi jumamosi.

Paul Kagame wa chama cha (RPF) ameibuka na ushindi kwa asilimia 98
Paul Kagame wa chama cha (RPF) ameibuka na ushindi kwa asilimia 98 REUTERS/Jean Bizimana
Matangazo ya kibiashara

Katika asilimia 80 ya kura zilizohesabiwa raisi Kagame amepata kiasi cha kura milioni 5.4 akivuka asilimia 51 zilizotakiwa ili mshindi kupatikana.

Tume ya uchaguzi imekadiria kufikia asilimia 97 ya kura milioni sita nukta tisa ya watu wote waliopiga kura.

Hata hivyo mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi nchini Rwanda Kalisa Mbanda amesema hatarajii matokeo hayo kubadilika hata baada ya kuhesabu asilimia zote za kura.

Aidha mgombea Frank Habineza wa chama pekee kilichoruhusiwa kufanya upinzani nchini humo cha Democratic Green amejipatia asilimia 0.45 ya kura huku mgombea binafsi Philippe Mpayimana akipata 0.72.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.