Pata taarifa kuu
RWANDA-UCHAGUZI-SIASA

Wanyarwanda wanapiga kura kumchagua rais wao

Raia wa Rwanda wanapiga kura leo Ijumaa kumchagua rais wao, katika Uchaguzi ambao dalili zote zinaonesha wazi kuwa rais Paul Kagame atachaguliwa tena kwa muhula wa tatu wa miaka saba.

Katika mitaa mjini Kigali, wanajianda kwenda kupiga kura kumchagua rais wao.
Katika mitaa mjini Kigali, wanajianda kwenda kupiga kura kumchagua rais wao. MARCO LONGARI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais anaye maliza muda wake, Paul Kagame mwenye umri wa miaka 59, anapambana na wagombea wengine wawili, wasiofahamika sana, waliopata muda wa wiki tatu kuuza sera zao kwa raia wa nchi hiyo ya Afrika ya Kati.

Wachambuzi wa siasa wanaona kuwa itakuwa vigumu sana kwa mgombea wa chama cha Democratic Green Party Frank Habineza na mgombea binafsi Philippe Mpayimana kumshinda rais Kagame.

Wapinzani hao wote hawatarajiwi kumpa ushindani mkubwa Kagame ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2000.

Akiendeleza kampeni zake katika wilaya mbalimbali nchini humo, hata rais Kagame amekuwa akiwaambia wafausi wa chama chake cha RPF kuwa, ana uhakika asilimia 100 ya kushinda uchaguzi huu.

Wagombea wanaoshindana na Paul Kagame katika uchaguzi huo wanasema wafuasi wao wamenyanyaswa lakini chama tawala kina kana tuhuma hizo.

Wachambuzi wengi wanabaini kwamba, Kagame anajiona kama kiongozi  thabiti na msingi wa kurejesha amani nchini humo baada ya kusaidia kumaliza mauaji ya kimbari mwaka 1994.

Pia Paul Kagame anasifiwa kwa kukuza uchumi wa taifa hilo.

Mafanikio hayo pamoja na maendeleo makubwa yameonekana kuwavutia wapiga kura Milioni 6.9 ambao watashiriki katika Uchaguzi huo katika taifa hilo lenye maelfu ya Milima.

Hata hivyo wakosoaji wanamshutumu kwa kukandamiza upinzani na kuzuiwa uhuru wa kisiasa nchini.

Siku ya Alhamisi Wanyarwanda wapatao 44,000 wanaoishi nje ya nchi kama Korea Kusini, Uingereza na Marekani, walipiga kumchagua rais wao.

Rais wa sasa Paul Kagame wa chama cha RFP, Frank Habineza wa Democratic Green Party of Rwanda na mgombea binafsi Philippe Mpayimana wote kwa pamoja wamnamenyana katika kinyang'anyiro hiki cha urais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.