Pata taarifa kuu
RWANDA-UCHAGUZI

Rais Kagame atabiriwa kushinda Uchaguzi wa Ijumaa

Raia wa Rwanda watapiga kura siku ya Ijumaa, katika Uchaguzi ambao dalili zote zinaonesha wazi kuwa rais Paul Kagame atachaguliwa tena kwa muhula wa tatu wa miaka saba.

Rais Paul Kagame
Rais Paul Kagame REUTERS/Eric Vidal
Matangazo ya kibiashara

Kagame mwenye umri wa miaka 59, anapambana na wagombea wengine wawili, wasiofahamika sana, waliopata muda wa wiki tatu kuuza sera zao kwa raia wa nchi hiyo ya Afrika ya Kati.

Wachambuzi wa siasa wanaona kuwa itakuwa vigumu sana kwa mgombea wa chama cha Democratic Green Party Frank Habineza na mgombea binafsi Philippe Mpayimana kumshinda rais Kagame.

Akiendeleza kampeni zake katika wilaya mbalimbali nchini humo, hata rais Kagame amekuwa akiwaambia wafausi wa chama chake cha RPF kuwa, ana uhakika asilimia 100 ya kushinda uchaguzi huu.

Mtalaam wa siasa nchini Rwanda Christopher Kayumba ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP kuwa, Kagame anajiona kama kiongozi  thabiti na msingi wa kurejesha amani nchini humo baada ya kusaidia kumaliza mauaji ya kimbari mwaka 1994.

Mafanikio hayo pamoja na maendeleo makubwa yameonekana kuwavutia wapiga kura Milioni 6.9 ambao watashiriki katika Uchaguzi huo katika taifa hilo lenye maelfu ya Milima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.