Pata taarifa kuu
UGANDA

Watu 121 walitoweka nchini Uganda tangu mwezi Januari

Polisi nchini Uganda wanasema kesi 48 za watu kutoweka zimeripotiwa nchini humo kwa kipindi cha miezi sita iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, inaaminiwa kuwa watu 121 wamehusishwa katika biashara haramu ya binadamu kwa kipindi hicho.

Inaripotiwa kuwa, watu 78 walisafirishwa nje ya nchi huku wengine 43 wakitoweka katika mazingira ya kutatanisha nchini humo.

Hata hivyo, Polisi wanasema wamefanikiwa kuwaokoa watu hao waliotoweka.

Moses Binoga, msimamizi wa kitengo cha kushughulikia visa vya watu kupotea, amesema idadi kubwa ya watu waliotoweka na kupatikana ni wasichana.

Wasichana wnegi waliohojiwa wamekuwa wakilalamikia kuwa wamekuwa wakinyanyaswa kingono wanapopelekwa katika mataifa ya  Mashariki ya Kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.