Pata taarifa kuu
BURUNDI-UN-KAFANDO-USHIRIKIANO

Serikali ya Burundi yamuonya mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa nchi ya Burundi rais wa zamani wa BurkinaFaso Michel Kafando, amemaliza zaira yake Alhamisi Juni 29 ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu kuteueliwa kwake, ambapo baadae atatembelea katika nji jirani kukutana na mratibu katika mazungumzo ya warundi, Bejamini William Mkapa, kisha ataelekea nchini Uganda kukutana na msuluhishi Yoweri Kaguta museveni kabla ya kuhitimisha ziara yake katika makao makuu ya Umoja wa Afrika jijini Addis Abeba nchini Ethiopia.

Michel Kafando, rais wa zamani wa mpito wa Bukina faso (2014-2015), ambaye ni mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi. Picha ya mwezi Novemba 2015.
Michel Kafando, rais wa zamani wa mpito wa Bukina faso (2014-2015), ambaye ni mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi. Picha ya mwezi Novemba 2015. AFP PHOTO / FILIPPO MONTEFORTE
Matangazo ya kibiashara

Ni ziara ya "heshima" kwa ajili ya mawasiliano ya kwanza na serikali ya Burundi, nchi ambayo inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa tangu rais Pierre Nkurunziza kuamua kuwania kwa muhula wa tatu tangu miaka miwili iliyopita.

Mazungumzo ya kuiondoa nchi hyo katika mgogoro huo yamekwama, licha ya shinikizo kutoka kwa jumuiya ya kimataifa. Michel Kafando ameonywa viongozi wa Burundi kwenda kinyume na matakwa ya serikali ya Burundi. Itafahamika kwamba watangulizi wake walikataliwa na serikali shutma kwamba walikua wakiegemea upande wa upinzani na kutoa ripoti za uongo dhidi ya utawala wa Pierre Nkurunziza.

Msemaji wa rais, Claude Karerwa Ndenzako, amesem wana imani na Mwakilishi mpya wa Umoja wa Mataifa kwa Burundi. "Serikali ina imani na mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa, " alisema msemaji wa Nkurunziza. Lakini alimuonya kwamba kama hatafuata matakwa ya serikali ya Burundi hasa kutoketi kwenye meza ya mazungumzo na upinzani ulio uhamishoni unaotuhumiwa kuhusika na vurugu nchini humo, serikali ya Burundi haitosita kumkataa kama watanguluzi wake.

"Watangulizi wake hawajashindwa, lakini wakati mwingine, waliegemea upande wa upinzani. hivyo basi, tunaamini kwamba hatokua kama watangulizi wake na tunamuomba aheshimu sheria za Burundi na kusoma vizuri azimio la Umoja wa Mataifa ili kujaribu kufufua mazungumzo hayo yaliyokwama, " amesema Bw Karerwa Ndenzako.

Michel Kafando, ambaye ni mara ya kwanza anazungumza na vyombo vya habari baada ya kuteliwa kwake kwenye nafasi hiyo amesema mchakato wa kusaka amani ni "jitihada kubwa mno", huku akisema kuwa yuko tayari kufanya kazi na serikali ya Burundi kwa kutafutia suluhu mgogoro wa kisiasa nchini Burundi. "Mimi sina jipya. Kazi niliokubali kwa hakika ni ngumu. Nadhani katika mambo yote, ni lazima pia kufanya kazi hiyo kwa makubaliano na nchi unataka kusaidia, " ameongeza Bw Kafando.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.