Pata taarifa kuu
BURUNDI-UN-USALAMA

Michel Kafando azuru Burundi

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi, Michel Kafando, ambaye aliteuliwa hivi karibuni kwenye nafasi hiyo yuko ziarani nchini Burundi tangu siku ya Jumanne Juni 27. Anatazamiwa kukutana kwa mazungumzo Alhamisi hii na rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza.

Rais wa zamani wa Mpito wa Burkina Faso Michel Kafando, alieteuliwa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi azuu nchi hiyo.
Rais wa zamani wa Mpito wa Burkina Faso Michel Kafando, alieteuliwa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi azuu nchi hiyo. AFP PHOTO/PIUS UTOMI EKPEI
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano mchana, Michel Kafando alikutana Waziri wa Mambo ya Nje, Alain-Aimé Nyamitwe, ambaye alisema anaridhika ziara ya afisa huyo wa Umoja wa Mataifa. Hii ni ziara ya kwanza nchini Burundi, ambapo rais wa zamani wa Burkina Faso atakutana na serikali ya Bujumbura, kabla ya kuingia ajenda ya mazungumzo wiki ijayo. Michel Kafando anafanya ziara yake hiyo katika nchi ambayo iko katika mazingira magumu.

Michel Kanfondo hajaweka wazi ziara yake hiyo na kuamua kusalia kimya, wakati ambapo Waziri wa mambo ya Nje wa Burundi alisema akuridhika baada ya mkutano huo wa kwanza. Alain-Aimé Nyamitwe amemuelezea mjumbe mpya maalum wa Umoja wa Mataifa kama mtu mwenye hekima wa kusikiliza" wengine.

Michel Kafando alikutana kwa mazungumzo Jumatano mchana na kundi la wanadiplomasia nchini Burundi. Na hii leo mchana atakutana ana kwa ana na rais Pierre Nkurunziza.

Hatua yake ya kwanza nchini Burundi inaonekana kuridhisha serikali ya nchi hiyo. Kwenye akaunti ya Twitter ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Burundi, ambayo imehakikisha kwamba rais wa zamani wa Burkina Faso ameahidi "kuleta ufumbuzi wa Afrika" kwa mgogoro wa Burundi.

Lakini vyanzo vya kidiplomasia vinahakikisha kwamba Michel Kafando kulingana na uzowefu wakeatasaidia timu ya usuluhishi ya kikanda kwa kufufua mazungumzo ya kuondokana na mgogoro huo, mazungumzo ambayo yako njia panda. Hata hivyo serikali ya Bujumbura kinaendelea kuhakikisha kwamba amani imerejea nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.