Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI

Wakenya waanza kuhakiki taarifa zao katika daftari la kupiga kura

Wapiga kura nchini Kenya, wanaanza hivi leo kuhakiki majina yao na taarifa nyingine muhimu katika daftari la kupigia kura kuelekea Uachguzi Mkuu mwezi Agosti.

Wakenya wakishiriki katika zoezi la kujiandikisha kama wapiga kura mwaka uliopita.
Wakenya wakishiriki katika zoezi la kujiandikisha kama wapiga kura mwaka uliopita. allafrica.com
Matangazo ya kibiashara

Tume ya Uchaguzi imesema wapiga kura zaidi ya Milioni 19 wanatarajiwa kushiriki katika zoezi hili litakaloendelea kwa muda wa siku 30 zijazo.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Wafula Chebukati amesema zoezi hili pia litasaidia kulisafisha dafatri hilo ili kuwafahamu wapiga kura halisi watakaoshiriki katika uchaguzi huo.

Inakadiriwa kuwa baada ya zoezi hili kumalizika, huenda majina Milioni 2 yakaondolewa katika daftari hilo kwa sababu mbambali ikiwa ni pamoja na kujisajili mara mbili.

Wakati uo huo, Tume ya Uchaguzi imeongeza muda kwa vyama vya siasa kuwasilisha majina ya wagombea wa nyadhifa mbalimbali hadi siku ya Jumapili.

Kampeni rasmi zinatarajiwa kuanz tarehe 28, huku wagombea urais wakitarajiwa kuwasilisha maombi yao mwishoni mwa mwezi huu.

Watu 18 wameonesha nia ya kuwania urais lakini pia ushindani mkubwa ni kati ya rais Uhuru Kenyatta na mgombea wa upinzani Raila Odinga.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.