Pata taarifa kuu

Vyama vya siasa vyaingia katika mchakato wa kutafuta wagombea Kenya

Vyama vyote vya siasa nchini Kenya vimeingia katika wiki muhimu ya kisiasa, kuwapata wagombea watakaopeperusha bendera ya vyama vyao wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti.

Vinara wa upinzani, kutoka kushoto, Moses Wetangula, Raila Odinga na Jonston Muthama.
Vinara wa upinzani, kutoka kushoto, Moses Wetangula, Raila Odinga na Jonston Muthama. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Tayari chama cha ODM kinachoongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, kimeanza mchakato huo katika kaunti mbalimbali.

Pamoja na hilo, vigogo wa muungano wa upinzani NASA, wanatarajiwa kukubaliana wiki hii kuhusu ni nani kati yao atakayepeperusha bendera ya upinzani dhidi ya rais Uhuru Kenyatta.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini humo Kadinali John Njue, ametoa wito kwa kampeni kufanyika kwa njia ya amani, na kuwataka vijana kutotumika kipindi hiki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.