Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Tume ya Uchaguzi na viongozi wa upinzani wakubaliana kuhusu kituo cha kujumuisha matokeo

Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, umeafikiana na Tume ya Uchaguzi IEBC kuhusu utaratibu wa upinzani kuwa na kituo chao cha kujumuisha matokeo ya urais wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti.

Wanasiasa wa upinzani wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi IEBC Wafula Chebukati Aprili 6 2017
Wanasiasa wa upinzani wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi IEBC Wafula Chebukati Aprili 6 2017 IEBCKenya
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kukutana na viongozi wa Tume ya Uchaguzi jijini Nairobi, imekubaliwa kuwa upinzani unaweza kuendelea na mpango wao wa kuwa na kituo cha kujumuisha matokeo lakini usitangaze matokeo.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Wafula Chebukati, amesema mawakala wa upinzani watakuwa na haki ya kisheria  kupata matokeo yote ya mwisho kutoka katika vituo mbalimbali lakini akasisitiza kuwa ni Tume tu ndiyo itakayokuwa na mamlaka  ya kutangaza matokeo ya mwisho.

Mwafaka huu unamaanisha kuwa, tofauti zilizokuwepo kati ya pande hizi  mbili zimetatuliwa na suluhu kupatikana.

Kigogo wa upinzani Raila Odinga na mwenzake Kalonzo Musyoka wamekuwa wakisisitiza kuwa upinzani umeweka mikakati ya kuwa na kituo chake cha kujumuisha matokeo na kuyatangaza na kusisitiza kuwa hakuna atakayewazuia kufanya hivyo.

Muungano wa NASA hivi karibuni umekuwa ukihoji utayari wa Tume ya Uchaguzi nchini humo na hata kusema hauwaamini Makamishena hao.

Hata hivyo, Tume ya Uchaguzi inasema zoezi hilo litakuwa huru na haki na ipo tayari kuandaa Uchaguzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.