Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Vigogo wa muungano wa upinzani nchini Kenya wakutana kumtafuta mgombea wa urais

Vigogo wanne wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, wanakutana Pwani ya nchi hiyo kujadiliana na kuamua ni nani kati yao atakayepeperusha bendera ya muungano huo wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti.

Wanasiasa wa upinzani nchini Kenya kuanzia kushoto Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi, Raila Odinga na Moses Wetangula
Wanasiasa wa upinzani nchini Kenya kuanzia kushoto Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi, Raila Odinga na Moses Wetangula RailaOdingaKE
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya watalaam waliokuwa wamepewa jukumu la kumtafuta mgombea wa upinzani kumaliza kazi yao na kutoa mapendekezo yao kwa wanasiasa hao wanne kufanya maamuzi ya mwisho.

Wanasiasa hao wanaotafuta tiketi ya muungano huo kupambana na rais Uhuru Kenyatta anayetafuta muhula wa pili ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, aliyekuwa Makamu wa rais Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi na Waziri wa zamani wa Mambo ya nje Moses Wetangula.

Vyombo vya Habari nchini Kenya vinaripoti kuwa, duru kutoka katika kamati ya watalaam imependekeza kuwa Raila Odinga awe mgombea urais huku Kalonzo Musyoka awe mgombea mwenza wake kama ilivyokuwa mwaka 2013.

Musalia Mudavadi inapendekezwa kuwa awe Waziri Mkuu huku Moses Wentangula akipewa Uspika au kiongozi wa walio wengi bungeni ikiwa muungano huo utashinda uchaguzi huo.

Wanasiasa hao wanakutana kwa muda wa siku tatu zijazo, huku ikitarajiwa kuwa mgombea wa upinzani akitazamiwa kutangazwa wiki ijayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.