Pata taarifa kuu
SHERIA-UHURU

Bunge la Rwanda lapitisha sheria inayodhibiti mashirika yasiyo ya kiserikali

Mswada wenye utata, unaodhibiti kikamilifu utendakazi wa mashirika yasiyo ya kiserikali, ulipitishwa siku ya Alhamisi mara ya kwanza kusomwa na Bunge nchini Rwanda, miezi michache kabla ya uchaguzi wa urais na wabunge.

Muswada huo umepitishwa kwa kura 45 za ndio na hakuna iliyoupinga, katika Bunge linalodhibitiwa kwa kiasi kikubwa na chama tawala cha Rwandan Patriotic Front (RPF).
Muswada huo umepitishwa kwa kura 45 za ndio na hakuna iliyoupinga, katika Bunge linalodhibitiwa kwa kiasi kikubwa na chama tawala cha Rwandan Patriotic Front (RPF). © AFP
Matangazo ya kibiashara

Wapinzani wa mradi huu, ambao lazima urudi kwa wabunge hivi karibuni kwa kura ya mwisho, wanaeleza kuwa unaweka mipaka ya uhuru wa kiraia katika nchi ambayo Rais Paul Kagame anatuhumiwa kutawala katika mazingira ya hofu, kukandamiza upinzani na uhuru wa kujieleza. Muswada huo ulipitishwa kwa kura 45 za ndio na hakuna iliyoupinga, katika Bunge linalodhibitiwa kwa kiasi kikubwa na chama tawala cha Rwandan Patriotic Front (RPF). Rasimu hiyo inapanga kuweka sheria kali juu ya utendakazi wa madhirika yasiyo ya kiserikali na haswa inayataka kuwasilisha bajeti yao ili kuidhinishwa na mamlaka ya Rwanda.

Rasimu hii "itapunguza nafasi ya kiraia kwa sababu inampa mbunge uwezo wa kuingilia usimamizi wa kila siku wa mashirika yasiyo ya kiserikali, ikiwa ni pamoja na kuwafuta kazi wafanyakazi," mkuu wa Jukwaa la Mashirika ya Kiraia ya Rwanda, Joseph Nkurunziza, ameliambia shirika lahabari la AFP. Anahofia kuwa mswada huo utapitishwa kwa haraka, huku uchaguzi wa urais - ambapo Paul Kagame anapewa nafasi kubwa ya kushinda - na uchaguzi wa wabunge uliopangwa kufanyika Julai 15 ukimaanisha kuvunjwa kwa Bunge katikati ya mwezi Juni.

Kulingana na mpinzani mwingine wa mswada huo, ambaye alitaka kutotajwa jina, rasimu hii inaweza kutumika kukatisha tamaa mashirika ya kiraia kudhibiti zoezi la kupiga kura na utendakazi wa tume ya uchaguzi na matafi yake yote mikoani na wilayani. Waziri katika ofisi ya rais, Judith Uwizeye, kwa upande wake alitetea mradi huo mbele ya Bunge siku ya Alhamisi, akithibitisha kuwa utafanya uwezekano wa kupambana dhidi ya mashirika "yasiyo ya maana" na "yanayopotosha" ambayo hayatimizi majukumu yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.