Pata taarifa kuu
BURUNDI-AMISOM

Burundi yatishia kuwaondoa askari wake nchini Somalia

Serikali ya Burundi kupitia Waziri wa Ulinzi, Emmanuel Ntahomvukiye, imetishia kuondoa wanajeshi wake wanaohudumu katika kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Somalia (AMISOM).

Wanajeshi wa Burundi wa kikosi cha Amisom, wakipiga doria katika wilaya ya Deynille, nchini Somalia, Novemba 18 mwaka 2011.
Wanajeshi wa Burundi wa kikosi cha Amisom, wakipiga doria katika wilaya ya Deynille, nchini Somalia, Novemba 18 mwaka 2011. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Burundi inasema uamuzi wa kuwaondoa askari wake nchini Somalia uko mbioni kuchukuliwa iwapo umoja wa ulaya hautojirudi na kutengua uamuzi wake wa kutopitisha mishahara ya wanajeshi hao mikononi mwa serikali.

Wanajeshi 5,500 wa Burundi wanahudumu katika kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Somalia, na ni nchi ya pili kwa wanajeshi wengi nchini Somalia, baada ya Uganda.

Mbele ya wabunge, Waziri wa ulinzi Emmanuel Ntahomvukiye amesema wanajeshi waliotumwa nchini Somalia hawajapata mishahara yao kwa muda wa miezi kumi.

Itafahamika kwamba kila mwanajeshi kutoka Burundi anapokea Dola 800 kila mwezi.

Wadadisi wanasema serikali ya Burundi imeamua kusema hivo baada ya kuona kwamba Umoja wa Ulaya, hasa Ubelgiji imeendelea kushikilia uamuzi wa kutopitisha mishahara ya askari wa Burundi waliotumwa nchini Somalia mikononi mwa serikali.

Ikiwa Umoja wa Ulaya itakataa kurejelea uamuzi wake, itakua pigo kubwa kwa Burundi kwani serikali ya nchi hiyo imekua ikinufaika kupitia fedha hizo zinazotolewa na Umoja wa Ulaya, mfadhili mkuu wa kikosi cha AMISOM, wamesema wadadisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.