Watu kadhaa wauawa Mandera, Kenya
Watu waliojihami kwa silaha wameshambulia mtaa mmoja mjini Mandera, nchini Kenya. Watu kadhaa wanahofiwa kuwa wameuawa katika shambulizi hilo. Serikali inawatafuta waliohusika na mauaji hayo, lakini imewanyooshea kidole cha lawama wapiganaji wa Al Shabab.
Imechapishwa:
We have suffered another Sad attack in mdr where six 6 have been confirmed killed one seriously injured. We grieve with our families.
— HE Capt. Ali I Roba (@aliiroba) October 6, 2016
Thanks to the timely response by our security teams, 27 out of 33 occupants of a plot were saved unhurt. Sadly 6 lives are too many to loose
— HE Capt. Ali I Roba (@aliiroba) October 6, 2016
Eneo la Mandera ilmekua likishambuliwa mara kwa mara na wapiganjai wa Al Shabab kutoka nchi jirani ya Somalia.
Mkuu wa jimbo la Mandera Ali Roba ameandika kwenye Twitter kwamba watu 6 wameuawa na mmoja kujeruhiwa. Lakini mashahidi wanasema idadi hiyo inaweza kuzidi kwani wanahofia kuwa watu zaidi ya kumi huenda waliuawa katika shambulizi hili.
Itakumbukwa kwamba wanajeshi wa Kenya wamekua wakitumwa nchini Somalia ili kuzima mashambulizi ya mara kwa mara nchini mwake na kuisaidia serikali dhaifu ya Somalia kuimarisha usalama nchini Somalia.