Pata taarifa kuu
KENYA-AL SHABAB

HRW yatwika lawama maafisa wa usalama Kenya

Ripoti ya Shirika la Kimataifa la kutetea haki za Binadamu la Human Rights Watch, inawashtumu maafisa wa usalama nchini Kenya kuwauawa na kuwateka washukiwa wa kundi la kigaidi la Al- Shabab Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Askari wa Kenya katika mpaka na Somalia.
Askari wa Kenya katika mpaka na Somalia. © STRINGER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Human Rights Watch inasema, watu 34 wametoweka na wengine 11 kuuawa kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita katika majimbo ya Garrisa, Mandera na Wajir.

Ripoti ya Shirika hilo inasema kutoweka na kuuawa kwa watu hao kumetokea kutokana na sera ya serikali ya Kenya ya kupambana na ugaidi kutumia kikosi maalum cha ATPU.

Kundi la Al-Shabab limekua likinyooshewa kidolea kuhusika na mashambulizi mbalimbali katika maeneo tofauti ya nchi ya Kenya, hasa maeneo yanayopakana na nchi jirani ya Somalia.

Hayo yakijiri, zaidi ya mabweni ya shule 100 za sekondari yameteketezwa moto katika mazingira ya kutatanisha huku maafisa wa polisi wakiwakamata mamia ya wanafunzi kwa madai ya kuhusika katika miezi kadhaa iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.