Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI

Marekani yasikitishwa na ripoti za kuteswa kwa wanaharakati nchini Sudan Kusini

Marekani imesema inasikitishwa sana na ripoti kutoka nchini Sudan Kusini kuwa wanaharakati wanateswa na wanaishi kwa hofu baada ya kukutana na wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wiki iliyopita.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (Kushoto), akiwa na Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Samantha Power (Kulia) alipozuru Juba hivi karibuni
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (Kushoto), akiwa na Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Samantha Power (Kulia) alipozuru Juba hivi karibuni REUTERS/Jok Solomun
Matangazo ya kibiashara

Samantha Power, Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa aliyekuwa miongoni mwa wajumbe waliozuru Sudan Kusini na kukutana na wanaharakati hao, amesema anasikitishwa sana na ripoti hizo.

Balozi huyo amesisitiza kuwa Marekani inalaani mateso au manyanyaso dhidi ya wanaharakati hao, ambao wamekuwa wakiikosoa serikali ya Juba kutokana na hali ya kisiasa na usalama nchini humo.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linawasiliana na serikali ya Juba kuhakikisha kuwa wanaharakati hao wanakuwa salama na hawasumbuliwi wala kunyanyaswa.

Ripoti zinasema kuwa, wanaharakati waliokutana na wajumbe hao wa Baraza la Usalama wametakiwa kufika mbele ya vyombo vya usalama na kujieleza.

Hadi sasa wanaharakati wawili wameshaondoka nchini humo kwa hofu ya kuuawa baada ya mwanaharakati mmoja kutoweka huku kukiwa na hofu kuwa ameuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.