Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI

UNSC yaidhinisha pendekezo la kutumwa kwa kikosi cha askari 4,000 Sudan Kusini

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limeidhinisha kupelekwa kwa kikosi imara cha askari 4,000 nchini Sudan Kusini baada ya makabiliano makali kurudisha nyuma juhudi za kumaliza vita kubwa nchini humo.

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakipiga kura.
Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakipiga kura. UN Photo/Loey Felipe
Matangazo ya kibiashara

Baraza hilo limepitisha azimio lililo pendekezwa na Marekani ambalo pia linatishia kuweka vikwazo vya silaha kwa Sudan Kusini ikiwa serikali itazuia kupelekwa kwa askari hao.

Nchi kumi na moja katika baraza hilo lenye wanachama 15 zilipiga kura kukubali azimio hilo lakini nchi za China, Urusi, Misri na Venezuela hazikupiga kura, kwa madai ya kushindwa kupata ridhaa ya Sudan Kusini kuhusu kupelekwa kwa kikosi hicho kipya.

Nchi za Ethiopia, Kenya na Rwanda zinatarajiwa kuchangia kwa wingi askari wapya ambao watakuwa na mamlaka ya "kutumia njia zote muhimu, ikiwa ni pamoja kuchukua hatua imara inapobidi" kutimiza wajibu wao.

Viongozi wa Afrika walitoa witowa kupelekwa kwa kikosi cha kikanda kulinda usalama katika mji wa Juba na kusaidia kulinda kambi za Umoja wa Mataifa baada ya kuzuka kwa vurugu katika mji mkuu Juba ambapo mamia ya watu walipoteza maisha mapema mwezi Julai.

 

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.