Pata taarifa kuu
UGANDA

Kamati ya bunge inayochunguza polisi nchini Uganda waukataa ujumbe wa Kayihura

Kamati ya Bunge kuhusu ulinzi na mambo ya ndani nchini Uganda imeufukuza ujumbe wa polisi uliofika mbele yake bila ya Inspekta Mkuu wa Polisi Jenerali Kale Kayihura jijini Kampala.

Inspekta Mkuu wa Polisi nchini Uganda Kale Kayihura
Inspekta Mkuu wa Polisi nchini Uganda Kale Kayihura Daily Moniter
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe huo ulioongozwa na Naibu Inspekta wa Polisi Martin Okoth Ochola na Andrew Felix Kaweesi ambao waliimbia Kamati hiyo kuwa walikuwa wanamwakilisha kiongozi wao.

Wabunge walikuwa wamejiandaa kumhoji Kaihura kuhusu utendakazi wa hivi punde wa jeshi la Polisi nchini humo baada ya kushuhudiwa kwa visa vya maafisa wa usalama wakiwapiga fimbo na kuwatesa wafuasi wa mwanasiasa wa upinzani nchini humo Kizza Beisgye.

Ujumbe huo wa Polisi ulijaribu kuwafafanualia wabunge hao kuwa kiongozi wao alikuwa amesafiri kwenda nchini Kenya kikazi lakini, hawakuweza kuwaridhisha.

Kanali Felix Kulaige ambaye pia ni mmoja wa wanakamati hao na anayewakilisha jeshi bungeni, alijaribu kumtetea Kayihura lakini utetezi wake ukaambulia patupu.

Majibizano makali yalizuka kati ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo Muwanga Kivumbi na ujumbe huo na kulazimu, polisi hao kuondoka pamoja na wanahabari.

Rais Yoweri Museveni wiki hii alisema hatua ya polisi kutumia nguvu dhidi ya wafuasi wa Besigye ni kwa sababu mwanasiasa huyo ameendelea kuwa msumbufu kwa kukataa kutii sheria za maafisa wa usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.