Pata taarifa kuu
UGANDA

Polisi wasema bado hawajaagizwa kufika Mahakamani kwa madai ya kuwatesa wafuasi wa Besigye

Polisi nchini Uganda inasema haijapokea maagizo yoyote kutoka Mahakamani kumtaka Inspekta Mkuu wa polisi Kale Kaihura kujibu madai ya polisi kutumia nguvu kupita kiasi na kuwatesa wafuasi wa mwanasiasa wa upinzani Kizza Besigye mwezi uliopita.

Maafisa wa usalama jijini Kampala, wakimkabili mfuasi wa Kizza Besigye hivi karibuni
Maafisa wa usalama jijini Kampala, wakimkabili mfuasi wa Kizza Besigye hivi karibuni Smithrise.com
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa polisi Fred Enanga amesema wiki moja baada ya tangazo hilo la Mahakama kutolewa na Mahakama ya Makindye jijini Kampala, hakuna kilichofanyika.

Aidha, amesema polisi inashtushwa na hali hii na inashuku kuna mchezo mchafu unaoendelea dhidi ya polisi Mahakamani.

Mbali na Kaihura, maafisa wengine wanaotarajiwa kuhojiwa ni pamoja na Andrew Kaggwa, kamanda za zamani wa Kusini kwa jiji la Kampala, pamoja na Kamanda Mkuu wa polisi jijini Kampala Samuel Bamuzibire miongoni mwa wengine.

Mahakama imepanga kuanza kusikiliza kesi hiyo tarehe 10 mwezi huu, baada ya kuwasilishwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu na raia wa kawaida.

Mawakili 20 wanatarajiwa kumkabili Kaihura ambaye anatuhumiwa kuwaagiza maafisa wa polisi kuwatesa wafuasi wa Besigye kwa kuwapiga viboko na kumgonga mwingine na gari la polisi.

Polisi wamekuwa wakijitetea kuwa wanalizimika kutumia nguvu kulinda amani jijini Kampala.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.