Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-MAREKANI

Marekani yawaonya wakuu wa Sudan Kusini, yataka mapigano yakome

Serikali ya Marekani, imetaka kusitishwa mara moja kwa vurugu nchini Sudan Kusini, baada ya kutokea mapigano mapya, jijini Juba, mapigano yanayotishia kuvunjika kwa mkataba wa amani kwenye taifa hilo jipya kabisa duniani. 

Balozi wa Marekani kwenye umoja wa Mataifa, Samantha Power
Balozi wa Marekani kwenye umoja wa Mataifa, Samantha Power UN Photo/Mark Garten
Matangazo ya kibiashara

Mapigano haya ni ya kwanza kati ya jeshi la Serikali na wanajeshi waasi mjini Juba, toka kurejea nyumbani kwa kiongozi wao, Riek Machar mwezi April mwaka huu, na kuchukua nafasi ya makamu wa kwanza wa Rais, kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu nchini humo kwa miaka 3.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, imeagiza kuondoka nchini humo kwa raia na wafanyakazi wake, na kulaani taarifa kuwa raia wa kawaida wemeshambuliwa, ambapo mpaka sasa watu 150 wamekufa kutoka kila upande.

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, akitia saini kwenye mkataba wa usitishaji wa mapigano nchini mwake, 26 August 2015
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, akitia saini kwenye mkataba wa usitishaji wa mapigano nchini mwake, 26 August 2015 UN Photo/Isaac Billy

Utawala wa Washington, unawataka viongozi wote wawili, wanasiasa na makamanda wa vikosi, kuagiza wanajeshi wao kujiepusha na makabiliano ili kuzuia mapigano zaidi, na kuagiza warudi kwenye makambi yao, amesema msemaji wa wizara hiyo, John Kirby.

"Marekani imedhamiria kuhakikisha inachukua hatua stahiki ili kuwawajibisha wahusika wa machafuko haya mapya ambayo ni wazi yanakiuka sheria za kimataifa zinazolinda binaadamu, ikiwemo kushambuliwa kwa kambi ya tume ya umoja wa Afrika nchini humo, UNMISS.

Machafuko haya yamejiri siku moja tu baada ya taifa hilo kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 5 toka taifa hilo lipate uhuru kutoka kwa Sudan, Jumamosi ya wiki iliyopita, Julai 9.

Makamu wa kwanza wa Rais wa Sudan Kusini, Riek Machar, Julai 8, 2015.
Makamu wa kwanza wa Rais wa Sudan Kusini, Riek Machar, Julai 8, 2015. REUTERS/Thomas Mukoya

Machafuko haya mapya yalianza Ijumaa ya wiki iliyopita na kuendelea hadi mwishoni mwa juma, ambapo wananchi wameonekana wakikimbia makazi yao mjini Juba, huku umoja wa Mataifa ukisema kuwa roketi na silha nzito za kivita zimetumiwa, halikadhalika ndege za kivita na vifaru.

Onyo hili la Marekani, linatolewa wakati huu baraza la usalama la umoja wa Mataifa, likifanya kikao chake cha dharula, ambapo umezitaka pande zote mbili kuzuia wanajeshi wao kukabiliana.

Nchi 15 wanachama za baraza la Usalama, zimewataka Rais Salva Kiir na makamu wake wa kwanza wa Rais Riek Machar, kuheshimu mkataba wa amani na kuhakikisha wanatekeleza maazimio ya usitishaji wa kudumu wa mapigano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.