Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-UN-MACHAR

Sudan Kusini: UN yatoa wito kwa uundwaji haraka wa serikali ya umoja

Umoja wa Mataifa umekaribisha kurudi kwa Riek Machar nchini Sudan Kusini. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wametoa wito kwa nchi hiyo kusonga mbele na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa haraka iwezekanavyo, wakibaini kwamba ni hatua muhimu kuelekea katika amani.

Riek Machar katika mkutano na waandishi wa habari alipowasili katika uwanja wa ndege Juba Aprili 26, 2016.
Riek Machar katika mkutano na waandishi wa habari alipowasili katika uwanja wa ndege Juba Aprili 26, 2016. © REUTERS/Jok Solomun
Matangazo ya kibiashara

"Huu ni ujio mpya bora wa Sudan Kusini kwa muda mrefu", mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Samantha Power, amekaribisha. Wajumbe kumi na tano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamebaini hasa kwamba, hatua mpya katika utekelezaji wa mkataba wa amani uliosainiwa Agosti 26, 2015 na nafasi kubwa ya kuanzisha mchakato wa amani baada ya miaka miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe viliyoharibu sehemu kubwa ya nchi.

Kuapishwa kwa Makamu wa rais Riek Machar ni lazima kufuatiwe na hatua nyingine, Umoja wa Mataifa umeonya. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameomba serikali ya umoja wa kitaifa iundwe haraka iwezekanavyo. Mwakilishi wa Sudan Kusini katika Umoja wa Mataifa amemuahakikishia Ban Ki-moon kuwa jambo hilo linapaswa kufanyika haraka iwezekanavyo. "Serikali ina nia thabiti ya kutekeleza makubaliano ya amani na serikali ya umoja wa kitaifa inaweza kuwa imeundwa ndani ya siku siku moja au mbili," amejibu.

Umoja wa Mataifa unakaribisha kurudi kwa hatua hiyo katika mchakato wa amani, lakini serikali ndio itaonyesha nia yake njema katika utekelezaji wa mkataba huo na kupatikana kwa amani ya kudumu nchini nzima.

Genevieve Garrigos, kiongozi wa shirika la kimataifa la Haki za binadamu la Amnesty International nchini Ufaransa akihojiwa na RFI, amesema kurudi kwa riek Machar ni hatua muhimu, ingawa bado kuna mengi ya kufanyika. "Itabidi kuona jinsi gani hatua zingine za mpango huo zitatekelezwa, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa tume ya "Ukweli, Maridhiano na Uponyaji", ambayo itashughulikia uhalifu mkubwa kabisa ulioofanywa na pande zote katika kipindi cha miaka miwili ya machafuko. Maelfu ya raia waliuawa, leo bado kuna wakimbizi zaidi ya milioni mbili, ikiwa ni pamoja na wakimbizi wa ndani. Itabidi watu wote waliohusika katika uhalifu huo wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria, vinginevyo tutakwenda katika mzunguko wa kutokuadhibu, hali ambayo inaweza kuibua vitendo vyaulipizaji kisasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.