Pata taarifa kuu
BURUNDI-USALAMA

Afisa wa ngazi ya juu katika jeshi la Burundi auawa Bujumbura

Jenerali Athanase Kararuza, ameuawa mapema asubuhi katika tarafa ya Gihosha, kaskazini mashariki mwa mji wa Bujumbura, alipokua akielekea kazini. Jenerali Kararuza ni kutoka jeshi la zamani lililokua likitawaliwa na Watutsi (FAB). Walioendesa shambulio hilo mpaka sasa hawajajulikana.

Afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la Burundi Brigedia Jenerali Athanase Kararuza akizungumza na waandishi wa habari, Februari 5, 2014.
Afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la Burundi Brigedia Jenerali Athanase Kararuza akizungumza na waandishi wa habari, Februari 5, 2014. © AFP/ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Mshauri mkuu wa Rais wa Burundi katika masuala ya mawasiliano, Willy Nyamitwe, ameandika kwenye Twitter akisema kwamba wale ambao wamemuua mwenzangu jenerali Kararuza na mashambulizi mengine kama hayo wana lengo la kuvigawa vyombo vya ulinzi (FDN) na usalama (PNB).

Hayo yanajiri wakati ambapo Waziri wa Haki za Binadamu, Martin Nivyabandi, na mkewe waliponea chupuchupu kuuawa katika shambulizi la Jumapili Aprili 24 saa sita mchana. Wote wawili walijeruhiwa katika shambulizi hilo la guruneti wakati ambapo walikua wakitokea kanisani mjini Bujumbura.

Taarifa hii kwanza ilianza kuzunguka katika mitandao mbalimbali ya kijamii kabla ya kuthibitishwa na Mkuu wa mji mkuu wa Burundi, nchi ambayo inaendelea kukumbwa na mgogoro ambapo mashambulizi ya hapa na pale yanayowalenga kwa mstari wa mbele viongozi kutoka pande zote yameongezeka.

Ni mwaka mmoja sasa baada ya kuanza kwa mgogoro uliyotokana na uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu. Kwa sasa viongozi wengi serikalini wanahofia maisha yao. hata rais wa nchi hiyo amekua akihofia maisha yake, kwani sasa anatumia muda mfupi katika mji mkuu, ulio na idadi kubwa a wafuasi wa upinzani na kuamua kutumia muda wakemrefu mjini Gitega, katikati mwa Burundi, kilomita zaidi ya 100 na mji wa Bujumbura.

Waziri Martin Nivyabandi na mkewe waliponea kwa miujiza kama inavyosema Mku wa jiji la Bujumbura, Freddy Mbonimpa. Guruneti ililipuka karibu na gari lao na kuvunja vioo vya gari hilo wakatiwalipokuwa wakilikaribia. Haijulikani iwapo magari yaliokuwa pembezeno mwa eneo walio kuwa wamesimama ndio yalizuia machicha ya guruneti hiyo kuowafikia. Mku wa jiji la Bujumbura anahakikisha kwamba "Mungu ndiye aliwalinda".

Freddy Mbonimpa pia amelaani "shambulizi la kigaidi ambalo limelenga mahali pa ibada". Amehusisha shambulio hilo kwa "wahalifu wenye silaha", maneno yanayotumiwa na viongozi wa serikali ya Burundi kwa kuwataja viongozi wa makundi ya waasi nchini Burundi, yalioanzishwa baada ya maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza.

Kwa mwaka mmoja sasa, viongozi wengi wa kisiasa, kijeshi na polisi, viongozi wa upinzani na viongozi wa vyama vya kiraia nchini Burundi wameuawa au wamenusurika katika mashambulizi.

Uhalifu huu unatekelezwa na pande zote mbili nchi humo, kwa mujibu wa vyanzo vingi, hata kama pande hizo bado hazijakiri kuhusika na uhalifu huo, zimekua zikitupiana lawama.

Hata hivyo raia mjini Bujumbura, na katika baadhi ya mikoa nchini humo wanaishi kwa hofu ya kuuawa, hasa usiku, huku wakijizuia kutembelea katika maeneo ya kunakokusanyika watu wengi, kama vile baa, na migahawa mbalimbali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.