Pata taarifa kuu
BURUNDI-UN-HAKI ZA BINADAMU

Burundi: kesi mpya 345 za mateso tangu mwanzoni mwa mwaka 2016

Nchini Burundi, vitendo vya unyanyasaji, mateso na ukatili katika jela mbalimbali vimeongezeka kwa kasi.

Bujumbura, Februari 3, 2016. Burundi, mzunguko wa vurugu na ukandamizaji vinandelea kushuhudiwa kwa mwaka mmoja sasa.
Bujumbura, Februari 3, 2016. Burundi, mzunguko wa vurugu na ukandamizaji vinandelea kushuhudiwa kwa mwaka mmoja sasa. © REUTERS/Jean Pierre Aime Harerimana
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, vitendo hivi vinaonekana kushika kasi kwa sababu tangu mwanzoni mwa mwaka 2016, kesi mpya 345 za mateso ziliorodheshwa na kufikia karibu 600, idadi ya vitendo vilivyoorodheshwa na Umoja wa Mataifa tangu kuanza kwa mgogoro nchini humo.

Ofisi ya Haki ya za Binadamu ya Umoja wa Mataifa pia ina wasiwasi kuhusu kuwepo kwa mahali pa siri wanakozuiliwa watu wanaokamatwa.

Katika jela inayojulikana rasmi, kama vile katika majengo ya Idara ya Ujasusi, zaidi ya nusu ya watu wanaozuiliwa sehemu hiyo wamefanyiwa mateso. Timu za Umoja wa Mataifa zilitembelea majengo hayo na ziliweza kushuhudiwa watu wengi wakiwa na majeraha makubwa ikiwa ni pamoja na kovu za kuchomwa kwa moto, viboko vya mikanda, vyuma au vitu vyenye ncha kali. Katika kesi nyingi, waathirika wananyimwa haki ya kupata huduma ya matibabu.

Ofisi ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inazungumzia nia ya kuficha ukweli, kwa kuwafungia ndani wafungwa ili wasiwezi kutoa siri, hadi majeraha yao kupona.

Pia Umoja wa Mataifa unawanyooshea kidole cha lawama viongozi mbalimbali wa vyombo vya usalama na kulaani "tabia ya kutoadhibu" kwa wahusika.

Waathirika wengi ni wanajeshi, hasa wanajeshi kutoka jeshi la zamani la Burundi (FAB), lililokua likiongozwa na idadi kubwa ya watu kutoka kabila la Watutsi. Kukamatwa, kupotezwa, mauaji, ni baadhi ya masaibu yanayowakuta wanajeshi kutoka jeshi la zamani (FAB), kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Hatimaye, licha ya kauli za viongozi ambao wamekua wakisema kuwa mambo yote yako sawa, Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imeorodhesha si chini ya mashambulizi thelathini yaliyotokea katika mji mkuu, kwa mwezi wa Machi pekee.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.