Pata taarifa kuu
BURUNDI-ITEKA-HAKI

Miezi 4 sasa tangu Marie Claudette Kwizera atoweke

Yupo wapi Marie Claudette Kwizera? Hilo ni swali ambalo shirika la haki za binadamu Ligue ITEKA nchini Burundi limekua likijiuliza baada ya mweka hazina wake kutoweka miezi minne iliyopita.

Ofisi ya shirika la Haki za Binadamu la Ligue ITEKA, Bujumbura, Burundi.
Ofisi ya shirika la Haki za Binadamu la Ligue ITEKA, Bujumbura, Burundi. © RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Marie Claudette Kwizera alitoweka tangu Desemba 2015, lakini kidole kimeendelea kunyooshewa Idara ya Ujasusi ya Burundi kuhusika na tukio hilo.

Mwezi Desemba 2015,Idara ya Ujasusi nchini Burundi iliamuru malipo ya kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kuachiliwa kwa mweka hazina huyo, malipo yasiyokua halali, na ambayo yamekithiri kwa Idara hiyo hiyo. Lakini leo sio tena suala la fedha. Idara ya Ujasusi inathibitisha kwamba haina taarifa yoyote kuhusu Marie Claudette Kwizera.

Hali hii inamtia wasiwasi hasa, Florent Geel, mkuu wa Ofisi ya Shirikisho la Kimataifa la Haki za Binadamu (FIDH) katika Ukanda wa Afrika: "Ni mtu ambaye alitoweka tangu mwezi Desemba 2015. Utafiti ulifanywa, hata ndani ya majengo ya Idara ya Ujasusi, ambayo ilisema hayijamuona Marie-Claudette Kwizera katika magereza. Wala hayupo katika gereza kuu la Mpimba mjini Bujumbura. Inamaanisha kwamba mtu huyu alitoweka. Ziarani nchini Burundi mwishoni mwa mwezi Machi, Shirikisho la kimataifa la Haki za Binadamu (FIDH) liliwataka viongozi mbalimbali wa kitaifa iliokutana nao, ikiwa ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ambaye hakuweza kujibu maswali yetu kuhusu hatima ya Marie-Claudette Kwizera au hata kusema kama uchunguzi ulianzishwa."

Hakuna taarifa yoyote kuhusu mfungwa huyo. Kwa mujibu wa Florent Geel, Marie-Claudette Kwizera alitekwa nyara kwa sababu ya jukumu lake kama mweka hazina, "Marie-Claudette alikua kisaini ripoti za fedha za shirika la haki za Binadamu la Ligue ITEKA, kabla na baada ya kusimamishwa kwa shirika hili, ikiwa ni pamoja na kusimamishwa kwa akaunti hizo za benki."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.