Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA-USALAMA

Burundi yaendelea kukumbwa na machafuko

Ni mwaka mmoja sasa tangu Burundi kutumbukia katika ghasia, huku juhudi za amani za kuliondoa taifa hilo dogo la Afrika ya Kati katika ghasia hizo zikikwama.

Askari wa Burundi wakiondoka katika kata ya Cibitoke, moja ya kitovu cha maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa Rais Nkurunziza à Bujumbura,Julai 1, 2015.
Askari wa Burundi wakiondoka katika kata ya Cibitoke, moja ya kitovu cha maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa Rais Nkurunziza à Bujumbura,Julai 1, 2015. MARCO LONGARI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Machafuko nchini Burundi yalianza baada ya maandamano makali kufuatia uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza wa kuwania katika uchaguzi wa rais katika muhula mwingine.

Vyama vya upinzani, mashirika ya kiraia pamoja na Kanisa Katoliki vilibaini kwamba Rais Nkurunziza hana haki ya kwania muhula mwengine, kwani atakua amevunja Katiba ya nchi na Mkataba wa Amani na Maridhiano wa Arusha, ambao ni muongozo mama kwa taifa la Burundi. Upinzani ulisema ukisisitiza kwamba iwapo Rais Nkurunziza atawania muhula mwingine, atakua ameliongoza taifa hilo kwa mihula mitatu, jambo ambalo ni kinyume na Katiba ya Burundi pamoja na Mkataba wa Amani na Maridhiano wa Arusha.

Hata hivyo, chama tawala na washirika wake walibaini kwamba Rais Nkurunziza hajavunja Katiba wala Mkataba wa Amani na Maridhiano wa Arusha, kwani ana haki ya kugombea muhula mwengine ambao, walisema ni wa pili, baada ya kuchaguliwa mara moja pekee na wananchi mwaka 2010.

Maandamano yageuka machafuko

Raia wakijawa na furaha katika mitaa mbalimbali ya mji wa Bujumbura, baada ya  jenerali Godefroid Niyombare kutangaza kuwuangusha utawala wa Pierre Nkurunziza Mei 13, 2015.
Raia wakijawa na furaha katika mitaa mbalimbali ya mji wa Bujumbura, baada ya jenerali Godefroid Niyombare kutangaza kuwuangusha utawala wa Pierre Nkurunziza Mei 13, 2015. REUTERS/Goran Tomasevic

Baada ya karibu mwezi mmoja wa maandamano makali mjini Bujumbura na katika baadhi ya mikoa, baadhi ya maafisa wa ngazi ya juu katika jeshi na polisi wakiongozwa na jenerali Godefroid Niyombare, Mkuu wa zamani wa Majeshi, walijaribu kufanya mapinduzi bila mafanikio, wakati Rais Nkurunziza alikua katika mkutano wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashiriki mjini Dar es Salaam, nchini Tanzania. Ilikua tarehe 13 Mei, 2015 saa saba mchana saa za Afrika ya Kati.

Baada ya kushindwa kwa jaribio hilo, Mei 14, 2015, serikali ilitangaza marufuku ya maandamano na kuwachukulia watu watakaoingia mitaani kama magaidi. Licha ya tamko hilo la serikali, maandamano yaliendelea na baadaye yaligeuka machafuko, baada ya vikosi vya usalama na ulinzi kujaribu kuzima maandamano hayo kwa kutumia silaha za moto.

Tangu wakati huo, polisi na jeshi ambavyo ni matunda ya Mkataba wa Amani na Maridhiano viligawanyika, huku baadhi ya wanajeshi na askari polisi wakitoroka Idara hizo na kujiunga na makundi ya waasi. Tayari vyombo vya usalama na ulinzi vinavyomuunga mkono Rais Nkurunziza vimewapoteza maafisa kadhaa wa ngazi ya juu, zaidi ya watu 400 wameuawa kwa mujibu wa mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu, na watu zaidi ya 200,000 wameyahama makazi yao na kukimbilia nje ya nchi.

Mazungumzo yakwama

Licha ya juhudi za kimataifa za kuliondoa taifa hilo dogo la Afrika ya Kati katika machafuko hayo, bado hali inaendelea kuwa mbaya zaidi huku serikali ikikataa katu katu kufanya mazungumzo na upinzani, ikidai kwamba baadhi ya vyama vya upinzani viilihusika katika jaribio la mapinduzi.

Mazungumzo baina ya Burundi yazinduliwa rasmi nchini Uganda Jumatatu, Desemba 28, kupitia upatanishi wa rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni.
Mazungumzo baina ya Burundi yazinduliwa rasmi nchini Uganda Jumatatu, Desemba 28, kupitia upatanishi wa rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni. RFI-KISWAHILI

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.