Pata taarifa kuu
ADA-FDLR-USALAMA

Rwanda: kituo cha polisi cha Bugeshi chashambuliwa

Hali ya usalama imeanza kuzorota Kaskazini Magharibi mwa Rwanda. Watu wanaosadikiwa kuwa wapiganaji wa kundi la waasi wa Kihutu wa Rwanda (FDLR) wameendesha shambulio katika kituo cha polisi cha Bugeshi, Kaskazini Magharibi mwa Rwanda kwenye mpaka na mkoa wa Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Waasi wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR, kilomita 150 kaskazini mashariki mwa Goma, mwaka 2009.
Waasi wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR, kilomita 150 kaskazini mashariki mwa Goma, mwaka 2009. AFP/ Lionel Healing
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya Usalam na Ulinzi vimefahamisha kwamba wapiganaji wa kundi la waasi wa Kihutu wa Rwanda (FDLR) wameshambulia kituo cha polisi Bugeshi usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili. Jeshi linasema lina imani kuwa wapiganaji hao wameendesha shambulio hilo wakitokea katika ardhi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Msemaji wa jeshi la Rwanda Luteni kanali Rene Ngendahimana, amesema wapiganaji wanaokadiriwa kuwa kati ya 20 na 30 wa kundi la waasi wa Kihutu wa Rwanda (FDLR) wameingia Rwanda wakitokea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo wanaendesha harakati zao.

Hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu idadi ya waliokufa au kujeruhiwa lakini jeshi la Rwanda kwenye Twitter limesema kuwa linadhibiti eneo la Bugeshi. Pia jeshi limesema kuwa taarifa zaidi kuhusu shambulio hilo zitatolewa baadaye.

Hata hivyo taarifa ambazo zimekua zikirushwa kwenye mitandao ya kijamii zimearifu kuwa askari polisi wawili huenda walipoteza mnaisa katika shambulio hilo.

Si mara ya kwanza kituo cha polisi cha Bugeshi kinashambuliwa na watu wenye silaha. Mwezi Machi kituo hicho kilishambuliwa na watu wenye silaha waliotajwa na serikali kuwa wa piganaji wa kundi la waasi wa Kihutu wa FDLR. Wakati huo jeshi lilifahamisha kuwa lilimuua mpiganaji mmoja.

Hivi karibuni Rais Paul Kagame amezionya baadhi ya nchi jirani bila kuzitaja, kwamba zimekua zikiwakusanya wapiganaji wa kundi la waasi wa Kihutu wa FDLR kwa lengo la kuhatarisha usalama nchi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.