Pata taarifa kuu
RWANDA - BURUNDI - MZOZO

Rwanda yasema itawahamisha wakimbizi wa Burundi katika mataifa mengine

Serikali ya Rwanda inasema itawahamisha wakimbizi wa Burundi katika mataifa mengine baada ya madai kuwa inawapa mafunzo ya kijeshi kuuangusha utawala wa serikali ya rais Piere Nkurunziza.

Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo
Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo
Matangazo ya kibiashara

“Serikali ya Rwanda haraka iweszekanavyo itaanza kufanya kazi na Jumuiya ya Kimataifa, kuwapeleka wakimbizi hawa katika nchi ya tatu,' taarifa hiyo ilieleza.

Aidha, taarifa hiyo ya Louise Mushikiwabo imeeleza kuwa sababu nyingine ni kuhakikisha kuwa wakimbizi hao wanakuwa salama na kusaidia kupatikana kwa suluhu ya kisiasa nchini Burundi.

Wiki iliyopita, watalaam wa Umoja wa Mataifa walitoa ripoti ya kuihstumu Rwanda kuwapa mafunzo wakimbizi kutoka Burundi kwenda kupigana nchini mwao.

Serikali ya Bujumbura nayo imekuwa ikiishtumu Rwanda kwa kufadhili na kuwapa mafunzo makundi ya waasi ili kuzua machafuko.

Tuhma hizi zimekuwa zikikanushwa mara kwa mara na serikai ya Rwanda inayosema hakuna ushahidi kuonesha kuwa inachochea mgogoro wa Burundi.

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR, linasema wakimbizi 75,000 wamekimbilia nchini Rwanda.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.