Pata taarifa kuu
UNSC-AU-BURUNDI-USALAMA

UNSC yaunga mkono uamzi wa AU kwa Burundi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaunga mkono uamuzi wa Umoja wa Afrika wa kuanzisha uchunguzi kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu nchini Burundi na kuonyesha utayari wake kuchukua hatua.

Askari polisi akipiga doria katika mitaa ya Bujumbura, mji mkuu wa Burundi, mwishoni mwa mwezi Julai.
Askari polisi akipiga doria katika mitaa ya Bujumbura, mji mkuu wa Burundi, mwishoni mwa mwezi Julai. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Baraza hilo limetoa tamko hilo Jumatao wiki hii likielezea kusikitishwa kwake na ukosefu wa usalama kuongezeka pamoja na vurugu nchini Burundi tangu utata wa uchaguzi wa Rais Pierre Nkurunziza ambapo tayari watu wasiopungua 200 wamepoteza maisha, huku watu 200,000 wakiikimbia nchi hiyo.

Baraza la Usalam la Umoja wa Mtaiafa linalaani kwa nguvu zote ukiukwaji wa haki za binadamu na vitendo vya vurugu vinavyofanywa vikosi vya usalama pamoja na wanamgambo au makundi ya waasi, na kuongeza kuwa wahusika watawajibika kwa matendo yao.

Shambulizi la hivi majuzi dhidi ya jengo kituo cha vijana Kamenge anapoishi Askofu Mkuu Jean-Louis Nahimana, Mwenyekiti  wa Tume ya Ukweli na Maridhiano ya nchini Burundi, ni kielelezo tosha cha vurugu hizo kama alivyobainishwa mwenyewe katika mahojiano na RFI.

Tamko hilo la Baraza la Usalama lililoandaliwa kwa ari ya Ufaransa, linatoa wito kwa serikali kuanza mazungumzo na upinzani pamoja na wadau wengine katika Ukanda kufikia makubaliano ya ufumbuzi wa mgogoro uliopo, huku kupitishwa kwa andiko hilo kukitanguliwa na mazungumzo na China na Urusi, ambao wameuzungumzia mgogoro wa Burundi kuwa ni jambo ndani na kupinga vikwazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.