Pata taarifa kuu

CHADEMA washinda uchaguzi wa Arumeru Mashariki, Watanzania watakiwa kupanda miti

Mgombea wa Chama Cha CHADEMA katika Uchaguzi wa Ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nasari amefanikiwa kuibuka na ushindi kwenye kinyang'anyiro hicho na kumuangusha mpinzani wake kutoka CCM Sioi Sumari.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Msimamazi wa Uchaguzi huyo Gratian Kagenzi ametangaza matokeo hayo ambayo yanaonesha kuwa Nassari 32,972 na sabini na mbili wakati mpinzani wake mkubwa Sumari ameambulia kura 26,757.

Mapema Msimamizi huyo wa Uchaguzi Kagenzi alitoa onyo kwa wananchi kuwa watulivu wakati ambapo zoezi hilo linaendelea kutokana na kuwepo dalili ya vurugu.

Mkuu wa Operesheni ya Uchaguzi wa Jimbo la Arumeru Mashariki na Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi Afande Isaya Mburu amesisitiza kuwa hali ya usalama imeimarishwa.

Kwa matokeo hayo Jodhua Nassari anakuwa Mbunge Mteule wa Jimbo la Arumeru mashariki kuchukua nafasi iliyoachwa wazi kufuatia kifo cha Jeremiah Sumari.

Wakati huohuo Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Kayanza Peter Pinda ametaka kila mwananchi kuhakikisha kuwa anapanda miti ambayo itakua badala ya kuishia kupanda na kisha kuona wajibu wake umeishia hapo.

Waziri Mkuu Pinda ametoa kauli hiyo wakati wananchi wa Tanzania wakiadhimisha siku ya kupanda miti kitaifa kwa lengo la kukabiliana na hali ya jangwa ambayo inaanza kunyemelea mataifa ya Afrika Mashariki.

Kiongozi huyo amesema umefika wakati kwa kila mwananchi kufahamu jukumu la kutunza mazingira ni la kila mtu tofauti na wengine ambavyo wamekuwa wakifikiri hilo ni jukumu la serikali pekee.

 

 

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.